Mmoja kati ya viongozi wanane wa Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) nchini Kenya ametangaza kujiuzulu
wadhifa wake huo mapema leo Jumatano.
Akitangaza hatua yake hiyo Roselyn
Akombe amesema kuwa amechukua uamuzi huo kutokana kwamba hana imani
iwapo IEBC inaweza kusimamia uchaguzi wa tarehe 26 ya mwezi huu au la.
Amesema kuwa hataki kushuhudia fedheha ya kile kitakachofanyika baada ya
uchaguzi. Kadhalika Roselyn Akombe amesema kuwa, kwa kuzingatia kwamba
maisha ya Wakenya yako hatarini, ameamua kujiuzulu wadhifa wake kama
mmoja wa viongozi wa IEBC.
Akombe amebainisha kwamba Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) ni moja ya vyanzo vya mgogogro wa
hivi sasa nchini humo na kwamba tume hiyo imedhibitiwa na pande ambazo
hata hivyo hakuzitaja. Baada ya mahakama ya kilele kubatilisha matokeo
ya uchaguzi wa duru ya kwanza uliofanyika tarehe nane Agosti mwaka huu,
kiongozi wa upinzani anayewakilisha muungano wa NASA alitaka kuondolewa
viongozi wote wa IEBC akisema kuwa hana imani nao tena.
No comments:
Post a Comment