Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran
ameashiria kufanyika kura ya maoni ya kujitenga eneo la Kurdistan la
Iraq na kusema kuwa, adui amegonga mwamba katika njama yake ya kuunda
kile kinachodaiwa kuwa ni 'Mashariki ya Kati Mpya.'
Ayatullah Mohammad Ali Movahedi
Kermani, amesema hayo katika khutba zake za Sala ya Ijumaa hii leo hapa
mjini Tehran na amemshauri Masoud Barzani, rais wa eneo lenye mamlaka ya
ndani ya Kurdistan nchini Iraq afungamane na serikali kuu ya Baghadad
na awaombe radhi watu wa Iraq na pia asiandae uwanja wa utawala wa
Kizayuni wa Israel kuwa na ushawishi katika eneo hili.
Ayatullah Kermani amamuenzi marehemu
Jalal Talibani aliyekuwa rais wa Iraq ambaye aliaga duniani tarehe tatu
mwezi huu wa Oktoba na kusema: "Talibani daima alikuwa anatafakari
kuhusu uhuru, heshima na adhama ya Wairaqi wa kaumu zote."
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia
ameashiria uadui wa Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kuwa: "Hotuba ya
Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran imedhihirisha tena uadui wa
Marekani dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu."
Ayatullah Kermani ameendelea kusema
kuwa, wananchi wa Iran kamwe hawatasahau usaliti wa Marekani na kwamba
wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran watatoa jibu linalofaa kwa uadui wa
dola hilo la kibeberu.
Kabla ya khutba za Sala ya Ijumaa,
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurusbiha Madhehebu za
Kiislamu, Ayatullah Mohsen Araqi alizungumza na waumini na kusema, Ahul
Bayt wa Mtume SAW ni msingi wa umoja na mshikamano wa umma mzima wa
Kiislamu.
No comments:
Post a Comment