Mahakama ya Katiba ya Uhispania imefuta kikao
kilichokuwa kimepangwa kufanywa na Bunge la eneo la Catalonia kwa ajili
ya kutangaza rasmi kujitenga eneo hilo.
Uamuzi
huo wa kuzuia kikao cha Bunge la Catalonia kilichopangwa kufanyika siku
ya Jumatatu Ijayo umechukuliwa kutokana na wito wa baadhi ya vyama vya
siasa vilivyoitaka Mahakama ya Katiba ya Uhispania kuchukua uamuzi wa
haraka.
Mahakama
hiyo imemtahadharisha Spika wa Bunge la Catalonia, Carme Forcadell
kwamba atakabiliwa na mashtaka ya jinai iwapo atapuuza uamuzi huo.
Awali
mahakama hiyo ilipinga suala la kuitishwa kura ya maoni ya kujitenga
eneo la Catalonia huko Uhispania ikilitaja kuwa ni kinyume na katiba.
Hata hivyo viongozi wa eneo hilo walipuuza uamuzi huo na kuitisha kura
hiyo ambayo imeonesha kuwa, asilimia 92 wa wakazi wa Catalonia wanaunga
mkono suala la kujitenga na Uhispania.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy amemtaka kiongozi wa eneo la
Catalonia, Carles Puigdemont kutupilia mbali fikra ya kujitenga eneo
hilo la sivyo atakabiliwa na "shari kubwa zaidi".
No comments:
Post a Comment