Sunday, October 8, 2017

MERKEL ASEMA ATAFANYA MAZUNGUMZO YA KUUNDA SERIKALI YA MSETO

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema chama chake cha Christian Democratic Union (CDU) kitafanya mazungumzo na wajumbe wa vyama vya Waliberali (FDP) na chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira juu ya kuunda serikali ya Mseto. Bibi Merkel amesema, leo chama chake cha CDU kitafanya kwanza mazungumzo na chama ndugu cha Christian Social Union (CSU) na baada ya hapo ndipo watazungumza kuona jinsi ya kuunda serikali imara ya vyama vya CDU/CSU, Chama cha FDP na chama cha Kijani. Hata hivyo kansela Merkel amesema ni wazi kwamba jukumu hilo ni gumu sana.

No comments:

Post a Comment