Kimbunga Nate kimewasili katika eneo linaloishi watu
wachache la pwani katika eneo ambalo mto Mississippi unaingia baharini
jana Jumamosi na kushambulia pwani ya ghuba kwa upepo na mvua.
Kimbunga Nate kimewasili nchini Marekani
Wakati kimbunga hicho kinachokwenda kwa kasi kubwa kikielekea
katika pwani ya Mississippi, ambako kinatarajiwa kushambulia eneo
hilo na kutishia kusababisha mvua kubwa na mafuriko ambayo
yataharibu nyumba na biashara.
Kimbunga Nate kilitarajiwa
kupita mashariki mwa New Orleans, kikiepuka kuushambulia mji huo
kwa upepo wake mkali . Na kasi yake kubwa ilipunguza uwezekano wa
mvua kunyesha kwa muda mrefu ambazo zingeharibu mfumo dhaifu wa
kusukuma maji taka.
Mawimbi makubwa katika pwani ya Santa Rosa nchini Marekani
Pamoja
na hayo, mji huo ambao ni maarufu kwa pati za usiku kucha
uliwekwa katika amri ya kutotembea usiku, kuanzia saa moja jioni na
mitaa haikuwa imejaa watu kama ilivyo kawaida yake katika usiku wa
Jumamosi.
Miji katika pwani ya Mississippi kama Gulfport na
Biloxi ilikuwa katika tahadhari ya juu. Baadhi ya hoteli zilizoko
katika eneo la ufukwe na kasino watu waliondolewa. Kimbunga Nate
kilidhoofika kidogo na kilikuwa katika kiwango cha kimbunga namba
moja kikiwa na upepo unaokwenda kwa kasi ya kilometa 85 kwa saa
wakati kiingia katika eneo hilo ambalo linaishi watu wachache la
Plaquemines.
Watabiri wa hali ya hewa walisema inawezekana
kwamba kimbunga hicho kikaimarisha nguvu zake na kuwa katika
kiwango cha kimbunga namba mbili , lakini inaonekana uwezekano
huo kuwa mdogo wakati usiku ukiingia.
Matayarisho kabla ya kimbunga Nate kuwasili
Hali ya hatari yatangazwa
Kasi
ya kimbunga hicho ilitishia jamii inayoishi mabondeni kusini
mashariki mwa Louisiana , mashariki mwa kijiji cha wavuvi cha
Alabama cha Bayou la Batre.
"Iwapo kutakuwa na mafuriko tena,
haya ndio yatakuwa," amesema Larry Bertron wakati yeye na mke wake
wakijitayarisha kuondoka nyumbani kwao katika jamii ya
Braithwaite ya eneo la parishi ya Plaquemines ambayo huathirika
mara kwa mara na mafuriko.
Magavaan mjini Louisiana ,
Mississippi na Alabama wametangaza hali ya hatari. Majimbo hayo
matatu hayakupata madhara makubwa katika kipindi hiki cha
vimbunga.
Wakaazi wakishirikiana kujaza mchanga katika vigunia kuzuwia mafuriko kabla ya kimbunga Nate kuwasili
Maafisa
wamewaokoa watu watano kutoka katika maboti mawili katika wakati
wa mawimbi makubwa kabla ya kimbunga hicho kuwasili. Boti moja
ilipoteza ingini yake katika ziwa Pontchartrain na watu wawili
waliokuwamo katika boti hiyo waliokolewa.
Gavana wa
Louisiana John Bel Edwards amewahimiza wakaazi kufanya matayarisho
ya mwisho haraka na kusisitiza kwamba kimbunga Nate kitaleta
uwezekano wa upepo mkali ambao unaweza kusababisha mawimbi
makubwa yanayofikia futi 11 katika baadhi ya maeneo ya pwani.
No comments:
Post a Comment