Rais Vladmir Putin wa Russia amesema kuwa,
hali ya sasa ya eneo la Mashariki ya Kati imekuwa mbaya kutokana na
njama za baadhi ya madola katika kulisukuma eneo hilo kuelekea kwenye
maslahi yao binafsi.
Rais Putin aliyasema hayo
Alkhamisi ya jana na kuongeza kuwa, baadhi ya madola yanafanya njama
kupitia mapinduzi ya kijeshi na nguvu za kijeshi, kwa lengo la
kuyaelekeza matukio ya eneo la Mashariki ya Kati kwenda upande wa
maslahi yao binafsi. Amefafanua kuwa, hadi sasa baadhi ya nchi badala ya
kupambana na ugaidi, zinajaribu kuvuruga usalama na amani ya eneo hilo.
Rais Vladmir Putin ameongeza kuwa, katika uwanja huo Russia kwa
kushirikiana na serikali halali ya Syria na baadhi ya nchi za eneo,
zinapambana na magaidi kwa kufuata sheria za kimataifa.
Aidha Rais Putin ameashiria mgogoro wa
eneo la Peninsula ya Korea na kusema kuwa, ni lazima mgogoro huo
kutatuliwa kwa njia za amani. Akieleza kuwa, baadhi ya nchi zinatekeleza
njama kupitia njia za kisiasa kwa ajili ya kudhamini maslahi yao ya
kiuchumi, amesema kuwa, baadhi ya hatua za kisiasa zina malengo ya
kibiashara na kwamba lengo la vikwazo vilivyopitishwa hivi karibuni na
kongresi ya Marekani dhidi ya Russia, ni kuiondoa Moscow katika soko la
nishati barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment