Kiongozi wa upinzani, Daktari Kiiza Besigye akipandishwa kwenye gari la polisi baada ya kusambaratishwa maandamano
Jeshi la polisi nchini Uganda leo (Jumatano)
limepiga marufuku kile lilichokiita ni maandamano haramu ya kupinga
mpango wa kuondoa kipengee ya umri katika kugombea urais. Juhudi za
kuondoa kipengee hicho zina nia ya kumfungulia njia Rais Yoweri Museveni
kuendelea kubakia madarakani bila ya kufungwa na kipengee hicho.
Muswada
wa kuondoa kipengee cha umri wa kugombea urais kiliwasilishwa katika
bunge la Uganda mwezi uliopoita na hivi sasa wabunge wanajadiliana na
wananchi wa kawaida kutaka kujua maoni yao. Hata hivyo juhudi hizo
zimekumbwa na upinzani kutoka sehemu mbalimbali.
Msaidizi
wa Inspekta Mkuu wa Polisi wa Uganda, Assuman Mugenyi amesema kuwa,
majadiliano hayo yanaruhusiwa lakini si ruhusa kufanya maandamano yasiyo
na kibali, kuchochea machafuko, kufanya kampeni za chuki, kutumia
maneno ya kashfa na vitu kama hivyo.
Kwa
kawaida wapinzani hawapewi vibali vya kuandamana nchini Uganda na hii
ina maana kwamba maandamano yoyote ya wapinzani ni kinyume cha sheria.
Musenyi
ametoa amri kwa maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa wabunge wanafanya
mashauriano hayo kwa utulivu na amani tena katika majimbo yao tu.
Jana
usiku, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na kutumia risasi za
plastiki kutawanya mamia ya wapinzani wa kufutwa kipengee cha umri
kinachomzuia Museveni kugombea tena urais.
Rais
Yoweri Kaguta Museveni amekuwa akiitawala Uganda kwa miaka 30 sasa.
Umri wake hivi sasa ni miaka 73 wakati katiba ya Uganda imepiga marufuku
mtu kugombea urais akiwa na umri wa miaka 75.
Mkuu
wa mrengo wa upinzani katika bunge la Uganda, Winne Kiiza amesema kuwa,
amri hiyo ya polisi ni kinyume cha katiba na ameahidi kukabiliana na
amri hiyo kwa njia yoyote ile.
Hadi hivi sasa haijajulikana muswada huo utarejeshwa lini Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura.
No comments:
Post a Comment