Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia
ametangaza kuwa kila hatua itakayochukuliwai na Marekani dhidi ya
waandishi habari na vyombo vya habari vya Russia haitaachwa bila ya
jibu.
Dmitry Peskov amesema kuwa hatua
yoyote itakayopelekea kubanwa uhuru wa vyombo vya habari vya Russia nje
ya nchi haitasalia bila ya jibu; na kwamba hatua hiyo itafuatiliwa pia
na fikra za waliowengi na kwa njia za kisheria.
Katika fremu hiyo, Bunge la Russia
(Duma) limepasisha mswada dhidi ya vyombo vya habari vya Marekani
vinavyoendesha shughuli zake huko Russia. Bunge la Russia limetangaza
kuwa, limechukua hatua hiyo kama jibu kwa hatua za karibuni za Marekani
dhidi ya Televisheni ya Russia Today. Mwanasheria Mkuu wa Marekani siku
kadhaa zilizopita aliitaka televisheni hiyo ya Russia Today iwe
imejisali kama taasisi ya kigeni hadi kufikia tarehe 13 mwezi huu;
kinyume chake akaunti za fedha za televisheni hiyo zilizopo Marekani
zitafungwa.
No comments:
Post a Comment