Ikulu ya Rais wa Marekani, White House, imetangaza kuunga mkono jinai za utawala wa Saudi Arabia dhidi ya Yemen.
Katika taarifa siku ya Ijumaa, White House, pasi na kuashiria
indhari za taasisi za kimataifa kuhusu nafasi ya Marekani na muitifaki
wake , Saudia, katika kuleta maafa ya kibinadamu nchini Yemen, kwa mara
nyingine ilitangaza uungaji mkono wa Washington kwa Saudia na waitifaki
wake katika vita dhidi ya Yemen.
Taarifa ya Ikulu ya White House, kinyume na ukweli wa mambo, ilidai
kuwa utawala wa Saudia umefungua Bandari ya Al Hudayda na Uwanja wa
Ndege wa Sanaa.
Utawala wa Riyadh,ambao unadhibiti mipaka yote ya kimatiafa ya Yemen,
ulikuwa umeahidi kufungua Bandari ya Hudayda na Uwanja wa Ndege wa
Sanaa baada ya kufunga maeneo hayo mawili 24 Novemba na kwa msingi hiyo
kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Dunaini, WFP, limeonya kuwa
mamilioni ya watu wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya mauti kufuatia
mzingiro uliowekwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na hivyo kuzuia
misaada kuwafikia wanaohitajia.
Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015
kwa uungaji mkono wa Marekani kwa lengo la kuirejesha madarakani
serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na
kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh. Hivi sasa Saudia inzuia misaada
kuwafikia mamilioni ya watu wa nchi hiyo wanaokabiliwa na njaa.
Raia zaidi ya elfu 13 wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na
maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja
wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za
Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa
wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia
tokea mwezi Aprili mwaka huu.
No comments:
Post a Comment