Kiongozi wa mungano wa upinzani nchini
Kenya NASA, Raila Odinga anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Jamhuri ya
Kenya January 30, 2018 Kuapishwa huko kunatokana na
upinzani nchini Kenya kutokukubaliana na ushindi wa rais Uhuru Kenyatta
aliyechaguliwa mwishoni mwa mwaka uliopita, ingawa upinzani haukushiriki
duru ya pili ya uchaguzi baada ya matokeo ya uchaguzi wa awali
kukataliwa na mahakama.
Hata hivyo baadi ya wafuasi wa NASA
hawaungi mkono hatua hiyo. Pia wafuasi wa chama tawala cha Jubilee
wanapinga vikali kuapishwa kwa Raila Odinga kwa kudai kuwa huenda
machafuko yakatokea.
Tukio la kuapishwa kwa Odinga pia
linapingwa vikali na Wakenya waishio nje ya nchi hiyo. Kwa upande wa
jeshi la polisi nchini Kenya limeimarisha usalama mjini Nairobi katika
eneo lililoteuliwa kwa ajili ya tukio hilo la kipekee, na kusisitiza
kuwa hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kwenda eneo hilo, ingawa wafuasi
wengine wa NASA wanaandaa usafiri wa kuelekea maeneo ya Nairobi
kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa Odinga.
No comments:
Post a Comment