Askari wa Côte d’Ivoire wameendeleza ghasia licha ya mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kuwaomba radhi.
Duru za habari nchini humo
zimetangaza kwamba, mapigano ya siku kadhaa zilizopita kati ya
makundi ya jeshi, yamepelekea askari kadhaa kuuawa na wengine
kujeruhiwa.
Inafaa kuashiria kwamba miezi michache
iliyopita kuliibuka uasi wa askari katika mji wa Bouaké nchini Ivory
Coast kutokana na matatizo ya kiuchumi na kushindwa serikali kulipa
madai ya wafanyakazi na askari, matatizo ambayo yalienea pia katika
maeneo mengine ya Côte d’Ivoire.
Akiwa na Rais Alassane Ouattara, Mkuu wa
Mmajeshi nchini humo aliomba radhi kwa taifa kutokana na uasi wa askari
hao waliochafua usalama huku akiahidi kufanyika marekebisho jeshini
katika mwaka mpya. Uasi wa zamani ambao uliwajumuisha pia askari ambao
walikuwa wanataka kulipwa marupurupu yao, ulishika kasi zaidi mwezi
Januari na mwezi Mei mwaka jana na kuisababishia matatizo makubwa
serikali ya Yamoussoukro.
Karibu askari 1000 mwaka jana
waliachishwa kazi jeshini katika fremu ya marekebisho hayo. Mwaka
2011 Côte d’Ivoire ilikumbwa na vita vya ndani ambapo baada ya
makubaliano, askari kadhaa waasi walijiunga na jeshi ambapo kwa mujibu
wa viongozi wa serikali, askari hao ndio wamekuwa chanzo cha uasi tangu
mwaka jana hadi sasa.
No comments:
Post a Comment