Raia 30 wa Iran na wawili wa Bangladesh
wameripotiwa kutoweka baada ya meli ya mafuta na nyingine ya mizigo
kugongana mashariki mwa pwani ya China.
Wizara ya Uchukuzi ya China imesema meli ya mafuta ya
Iran yenye jina 'Sanchi' imegongana na meli ya mizigo yenye nambari ya
usajali ya Hong Kong inayoitwa “CF Crystal” mashariki mwa bahari ya
China katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Taarifa ya wizara hiyo imesema meli hiyo ya mizigo ya China iliyokuwa
na mabaharia 21 ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka na ilikuwa
ikitokea Marekani kuelekea katika mkoa wa Guangdong nchini China.
Wizara ya Uchukuzi ya China imesema mabaharia wake wote waliokuwa katika meli hiyo ya mizigo wameokolewa.
Habari zaidi zinasema kuwa, meli ya mafuta ambayo ilikuwa imebeba
tani 136,000 za mafuta kwa ajili ya Korea Kusini iliripuka na kuteketea
katika ajali hiyo.
Shirika rasmi la habari la Iran (IRNA) limethibitisha kuwa meli hiyo
ya mafuta ni milki ya nchii hii lakini ilikuwa imekodiwa na shirika
moja la Korea Kusini.
Polisi ya Baharini ya Korea Kusini inaongoza katika operesheni ya
uokoaji na kutafuta miili ya walipoteza maisha katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment