Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani
amesisitiza juu ya ulazima wa kuchukuliwa hatua za dhati za kukabiliana
na vitendo vya ubakaji na kunajisiwa watoto.
Papa Francis amesema hayo baada ya
kurejea kutoka katika safari yake ya Amerika ya Latini ambayo
iligubikwa na kashfa za ngono katika makanisa ya katoliki.
Sambamba na kutahadharisha kuhusiana na
vitendo vya kubakwa na kunajisiwa watoto wadogo amesisitiza kwamba,
wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Itakumbukwa kuwa, akiwa katika safari
yake nchini Chile, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani alieleza
masikitiko yake kutokana na kashfa za ngono na ulawiti zinazolikabili
kanisa hilo nchini humo.
Katika hotuba yake ya kwanza akiwa pamoja na Rais Michelle Bachelet
wa Chile, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani alisema kuwa, kashfa hizo
za ngono zimelipaka matope kanisa hilo.
Kashfa mbalimbali za kimaadili na
kifedha zilizoikumba Vatican na Kanisa Katoliki katika miaka ya hivi
karibuni zimekuwa zikigonga vichwa vya habari na kuwa gumzo kubwa
lisilokwisha duniani.
Kuna mamia ya kesi za ubakaji na ulawiti
zinazowakabili makasisi wa kanisa hilo, ambazo zimerundikana katika
mahakama za Ulaya na Marekani zikisubiri kufanyiwa uchunguzi, jambo
ambalo limeshusha hadhi ya Kanisa Katoliki Duniani.
No comments:
Post a Comment