Mkutano wa 32 cha Umoja wa Afrika (AU)
umeanza huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia kwa kuhudhuriwa na
viongozi wengi wa nchi za Kiafrika.
Vikao vya duru ya 32 ya Mkutano wa
Umoja wa Afrika vimeanza leo Jumapili kwa kuhudhuriwa na viongozi wengi
wa nchi za Afrika. Vikao hivyo vimeendeshwa katika hali ya faragha na
duru ya 32 ya Mkutano wa Viongozi wa Afrika imepangwa kufunguliwa baada
ya kumalizika vikao hivyo.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa ambaye anahudhuria katika mkutano huo amesisitiza kuwa ipo
haja ya kuungwa mkono nchi za bara la Afrika ili kuweza kuwa na amani na
kustawisha taasisi za nchi hizo. Guterres amesema kuwa, askari jeshi wa
Umoja wa Mataifa wataendelea na shughuli zao barani Afrika.
Duru ya 32 ya Mkutano wa Viongozi wa
Nchi za Afrika itadumu kwa siku mbili; ambapo washiriki katika mkutano
huo watajadili na kuchunguza mizozo na changamoto kuu zinazozikabili
baadhi ya nchi za Afrika, ugaidi, na suala la kuimarisha mashirikiano
kati ya nchi hizo chini ya kaulimbiu "Ushindi katika mapambano dhidi ya
ufisadi na mageuzi Afrika."
No comments:
Post a Comment