Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
linakutana leo Alkhamisi katika kikao chake cha dharura kwa shabaha ya
kujadili kadhia ya Palestina.
Tayseer Jaradat, Naibu Waziri wa
Mashauri ya Kigeni wa Palestina amesema kuwa, kikao hicho cha dharura
cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kinafanyika kwa ombi la
Palestina.
Riyadh Mansour, balozi na mwakilishi wa
kudumu wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, lengo la kikao
hicho ni kulikumbusha majukumu yake Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kuhusiana na Palestina.
Itakumbukwa kuwa, Disemba 21 mwaka jana,
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha kwa wingi wa kura azimio la
kuiunga mkono Beitul-Muqaddas.
Kwa mujibu wa azimio hilo, Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba,
hauitaimbua Beitu-Muddas kama mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel.
Tarehe 6 mwezi uliopita wa Disemba, Rais
Donald Trump wa Marekani aliitangaza Quds Tukufu kuwa eti ni mji mkuu
wa utawala pandikizi wa Israel na akatoa amri ya kufanyika taratibu za
kuuhamishia mjini humo ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv, mji mkuu wa
utawala dhalimu wa Kizayuni.
Hii ni katika hali ambayo, mji wa Quds
kunakopatikana Masjid Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu
isiyotenganishika na Palestina na ni miongoni mwa maeneo matatu muhimu
na matakatifu baada ya Makka na Madina.
No comments:
Post a Comment