Balozi
wa Tanzania nchi Ubelgiji Mh:Edward Joseph Sokoine katikati akiwa na
baadhi ya watanzania waliofika jana kwenye kikao cha kusikiliza na
kutafutia ufumbuzi kero za watanzania wanaishi mbali na Tanzania. {Picha
zote na Maganga One Blog}
Kiongozi
wa Watanzani kitongoji cha Antwerpen nchini Ubelgiji ndugu Joseph
Makani akimkaribisha Mh;Balozi na maafisa Ubalozi alioambana nao hapa
jana,kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi ndugu Shoo na upande wa kulia ni
afisa ubalozi ndugu Juma Salum.Kikao kilikwenda vizuri kwani kila mmoja
alipewa fursa ya kuuliza maswali.
Afisa
Ubalozi ndugu Juma Salum{kulia}akitoa ufafanuzi wa swali aliloulizwa
kuhusu maswala ya hati za kusafiria pindi mtu anapotaka kurudi
nyumbani,alielezea kwa kirefu taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili mtu
kuepuka usumbufu.
Mh:Balozi akimsikiliza mmoja wa watanzania ndugu Omari Songambele {hayupo pichani}aliyetaka ufafanuzi kuhusu Uraia Pacha.
Baadhi ya kina mama wa Kitanzania na nchi jirani walihudhuria mkutano uliowakutanisha na Balozi Sokoine
Na kwa upande wa kina baba nao walijumuika kwa wingi hapo jana kusikiliza na kutoa maoni kuhusu nchi yao
Mwenyekiti wa Watanzania nchini Ubelgiji ndugu Mwasha akijitambulisha kwa Mh:Balozi kabla ya kikao hakijaanza rasmi.
Afisa
ubalozi wa Tanzania ndugu Juma Salum,jana alipata nafasi nzuri ya
kuyajibu vizuri maswali ya watanzania. Pichani akiendelea kufafanua
jinsi ofisi ya balozi inavyofanya kazi zake vyema na kuwasaidia
watanzania kwa hali na mali pindi wanapohitaji msaada kwenye ofisi za
ubalozi.
Mmoja wa Watanzania ambaye anaishi nje ya nchi na amefaikiwa kuzaa na mzungu,Pichani wakimsikiliza Mh:Balozi
Pichani baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Mh:Balozi
Pichani baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Mh:Balozi
Mh:Balozi Sokoine akiwasisitiza Watanzania kuwekeza na kupeleka wawekezaji nyumbani
Afisa
balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ndugu Shoo akiwaeleza watanzania
Fursa za Hisa zitokanazo na mabenki makubwa nchini Tanzania na jinsi ya
kujiunga nazo
Afisa
Ubalozi wa Tanzania nduguKabakati nae aliongea na watanzania kuhusu
uwekezaji katika sekta mbalimbali,pichani alitoa ufafanuzi wa maswala ya
umiliki wa ardhi na mashamba
Afisa
ubalozi na Kanali mstaafu akiwashauri Watanzania kutokusahau walikotoka
na kuwasisitiza kuwekeza nyumbani,kutovunja sheria za nchi wanazoishi
Afisa
ubalozi na Kanali mstaafu akiwashauri Watanzania kutokusahau walikotoka
na kuwasisitiza kuwekeza nyumbani,kutovunja sheria za nchi wanazoishi
Watanzania,Wasomali,Warundi
, Wacongo na nchi nyingine za jirani kuizunguka Tanzania walihudhuria
mkutano wa Balozi wa Tanzania Mh:Balozi Sokoine hapo jana.
Maganga One Blogger akiwa na maafisa ubalozi wa Tanzania wakibadilishana mawazo
Maganga
One Blogger alipata fursa ya kuongea na Mh:Balozi na kumueleza
changamoto za Watanzania ughaibuni,Mh:Balozi Sokoine aliahidi kuwasaidia
Watanzania kadri atakavyoweza na kutatua kero zao.
Mh:Balozi
Sokoine akiagana na Omary Songambele mara baada ya kikao kumalizika
hapa jana.pembeni mwa balozi ni Dulla Criss Cross mmoja wa viongozi wa
Antwerpen
Shabiki namba moja wa Simba ughaibuni ndugu Nyambi kushoto akiwa na dada wa Kitanzania wakipata picha ya kumbukumbu
Kutoka
kushoto ni Afisa Balozi na kanali mstaafu,ndugu Omary
Songambele,Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Kassim Manara,Afisa
ubalozi ndugu Kabakati na Mh:Balozi Edward Sokoine hapo jana jijini
Antwerpen katika kikao cha kuzungumzia maendeleo ya nchi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment