Chanzo, DW.
Jeshi la Polisi nchini Ujerumani limewatawanya waandamanaji
takribani 15,000 wa kikurdi waliokuwa wamebeba mabango yanayoonesha
nembo za chama cha wafanyakazi wa Kikurdi PKK, zilizopigwa
marufuku nchini humo.
Katika taarifa zilizoripotiwa na shirika la habari la Ujerumani DW,
zilieleza kuwa Maandamano hayo yaliyofanyika mjini Kolon-Ujerumani,
yalitayarishwa na chama cha wafanyakazi cha NAV-DEM cha Wakurdi
ambacho kinaelezwa kuwa na ukaribu na chama kilichopigwa marufuku
cha PKK. Chama hicho kinaelezwa pia kupigwa marufuku nchini Uturuki
pamoja na washirika wake wa mataifa ya magharibi
kwamba ni kundi la kigaidi. Watu wawili walikamatwa katika
maandamano hayo, ambayo yaliyokuja
wiki moja baada ya vikosi maalum vya jeshi la
Uturuki na waasi ambao ni washirika wa Uturuki nchini Syria, kufanya
mashambulizi yakuwalenga wanamgambo wa Kikurdi wa kundi la vikosi
vya ulinzi wa umma YPG, kaskazini mwa Syria.
Hakuna tukio lililoripotiwa mara moja, japo hali iliripotiwa
kuendelea kuwa tete, kwa mujibu wa msemaji wa polisi ambaye aliongeza
kwamba kulikuwa na wasi wasi juu yakuzuka mapambano kati ya
waandamanaji na polisi.
No comments:
Post a Comment