Sunday, January 14, 2018

TRUMP ALIWALIPA WANAWAKE 100 WANYAMANZE KIMYA KUHUSU UHUSIANO HARAMU WA KIJINSIA

Trump aliwalipa wanawake 100 wanyamaze kimya kuhusu uhusiano haramu wa kijinsia
Rais Donald Trump wa Marekani aliwalipa pesa wanawake 100 ili wanyamaze kimya kuhusu uhusiano haramu wa kijinsia aliokuwa nao.
Steve Bannon, mshauri wa zamani wa Trump amenukuliwa katika kitabu cha Ghadhabu na Moto kilichoandikwa na Michael Wolff akisema kuwa, Trump alimtumia wakili wake wa muda mrefu, Marc Kasowitz 'kuwatuliza' wanawake 100 ili wasimharibie jina wakati wa kampeni za urais.
Hayo yanajiri wakati ambapo taarifa kwenye vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kwamba wakili wa rais Trump alimlipa mwigizaji wa filamu za ngono zaidi ya dola laki moja, kama njia ya kumshawishi asiseme lolote kuhusu zinaa ambazo inadaiwa alishiriki na Donald Trump.
Malipo hayo yalitolewa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa urais, katika wakati muhimu kwenye kampeni ya Trump, wakati alipokuwa anapuuza madai kwamba aliwadhalilisha wanawake.
Trump na mwanamke aliyemlipa kitita kikubwa cha fedha ili anyamaze
Gazeti la The Wall Street Journal linasema kwamba wakili huyo, kwa jina, Michael Cohen, alilipa pesa hizo baada ya Stormy Daniels, kutishia kufichua siri zake hadharani.
Gazeti la New York Times zinasema wakili huyo Michael Cohen alikanusha madai ya kukutana na Bi Stormy, japo hakutaja malipo yoyote.

No comments:

Post a Comment