Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika mji
mkuu wa India, New Delhi, kabla ya kuanza safari ya Waziri Mkuu wa
Israel, Benjamin Netanyahu katika nchi hiyo.
Makumi ya waandamanaji hao, aghalabu yao wakiwa vijana wa
Kiislamu jana Jumamosi waliteketeza moto bendera za utawala wa Kizayuni,
kulalamikia safari ya Netanyahu katika nchi yao.
Waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu wamekosoa vikali hatua ya hivi
karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kuitambua Quds Tukufu
kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
Baadhi ya vijana hao aidha wamechoma moto mabango yaliyokuwa na picha za Trump na Netanyahu.
Duru za habari zinasema kuwa, maandamano kama hayo ya New Delhi yameshuhudiwa katika vijiji zaidi ya elfu moja nchini India.
Netanyahu anatazamiwa kuanza safari ya kikazi ya siku sita nchini
India, licha ya New Delhi kupiga kura ya kuunga mkono azimio la Umoja wa
Mataifa la kupinga uamuzi wa Marekani wa kuitambu Quds kuwa mji mkuu wa
Israel.
No comments:
Post a Comment