Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
ametengua uteuzi wa Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na
kumteua Profesa Shukrani Manya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) kuwa Kamishna wa Madini nchini humo.
Magufuli
ametangaza uteuzi huo Jumatatu ya leo katika hotuba fupi aliyoitoa mara
baada ya kumwapisha Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini
wanchi hiyo. Katika hotuba hiyo Magufuli amesema: "Mambo ya ovyo ni
mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa
kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi.
Aidha amesema: "Yanayogundulika huko ni
ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na
pale Ubungo." Akielezea kutohitaji kuwabembeleza watendaji wa serikali
wanaofanya uzembe rais huyo wa Tanzania amesema: "Mimi si mwanasiasa
mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wa kubembeleza, ila
mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini)
ziwe zimesainiwa. Kadhalika Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na
namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu
yao polepole na bila ya kujali maslahi ya nchi hiyo mwanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment