Makumi ya maelfu ya Wapakistani wamefanya
maandamano katika miji tofauti ya nchi hiyo katikka kulalamikia matamshi
ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yao na
wameitaka serikali kumtimua balozi wa Marekani nchini humo.
Maandamano yameshuhudiwa katika
miji ya Lahore, Faisalabad, Hyderabad na miji mingine ya kusini mwa nchi
hiyo ambapo waandamanaji wamelaani siasa za kichokozi na kupenda
kujitanua za Trump dhidi ya mataifa mengine. Kadhalika waandamanaji hao
waliokuwa na hasira wamelichoma moto sanamu la rais huyo wa Marekani na
pia bendera ya nchi hiyo na kusisitiza azma yao ya kuitaka serikali ya
Islamabad kumtimua balozi wa Marekani nchini humo.
Hii ni katika hali ambayo Wizara ya
Mambo ya Nje ya Pakistan hivi karibuni ilimwita balozi wa Marekani
nchini humo David Hale katika kulalamikia tuhuma za hivi karibuni za
rais wake dhidi ya nchi hiyo. Mahusiano kati ya Pakistan na Marekani
yameharibika tangu mwezi Agosti mwaka jana baada ya Trump kuituhumu nchi
hiyo kwamba inawaunga mkono magaidi huku akitishia kuikatia misaada ya
kifedha.
No comments:
Post a Comment