Raia takriban 90 wa Somalia na
wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa
kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini
humo kinyume cha sheria.
Wote waliwasili katika uwanja wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, lakini baadaye raia wa
Somalia wakaendelea na safari hadi uwanja wa ndege wa Aden Abdulle mjini
Mogadishu.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia
BBC kwamba ni kweli raia hao wamefukuzwa Marekani, ingawa hakusema iwapo
hatua hiyo imetokana na msimamo wa Bw Trump..
"Ni watu 90
kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani
kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC.
Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani)," |
No comments:
Post a Comment