Sunday, January 1, 2017

JELA YAVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA BAHRAIN, WAFUNGWA WAACHIWA HURU

Watu waliokuwa na silaha wameivamia jela ya Jau nchini Bahrain na kumuua polisi mmoja na kuwatorosha wafungwa wa jela hiyo. Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain.
Shambulio hilo limefanywa leo na watu wenye silaha katika jela ya Jau ambako wanaharakati, wapinzani na raia waliokuwa wakiandamana dhidi ya serikali ya Manama walikuwa wamefungwa. Jela hiyo yenye sifa mbaya inapatikana kusini mwa mji mkuu wa Bahrain, Manama.
Mandhari ya ndani ya jela ya Jau huko Manama Bahrain 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imethibitisha katika taarifa hii leo kuwa, watu wenye silaha walioivamia jela hiyo wamemuua kwa kumpiga risasi askari polisi aliyetambulika kwa jina la Abdul Salam Saif na kusababisha wafungwa kadhaa kutoroka. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain imeongeza kuwa jeshi tayari limeanza kuwasaka watu waliohusika na shambulio katika jela ya Jau huko Manama pamoja na wafungwa waliotoroka. Itafahamika kuwa maelfu ya wanaharakati wamefungwa jela huko Bahrain kwa tuhuma mbalimbali kuanzia kushiriki katika maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa na kuvishambulia vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment