Monday, January 2, 2017

GALLUP: WAMAREKANI WANASHUKU UWEZO WA TRUMP WA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

Wamarekani waliowengi wana shaka kuhusu uwezo wa rais mteule wa nchi hiyo wa kutekeleza majukumu yake.
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Gallup yanaonesha kuwa, zaidi ya nusu ya Wamarekani wanaamini kwamba rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump hawezi kusimamia migogoro mbalimbali ya kimataifa.
Matokeo ya uchunguzi wa Gallup yanasema kuwa, asilimia 53 ya Wamarekani wanaamini kuwa, Trump hataweza kutumia jeshi la Marekani kwa njia za kimantiki.
Trump
Doland Trump
Matokeo hayo yanaoana na yale yaliyofanywa awali na taasisi hiyohiyo ya uchunguzi wa maoni ambayo yalionesha kuwa, kwa ujumla Doland Trump ana umashuhuri na uungaji mkono mdogo zaidi akilinganishwa na marais waliotangulia wa Marekani.
Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa baina ya tarehe 7 hadi 11 Disemba yalichapishwa jana katika mtandao wa Gallup.

No comments:

Post a Comment