Wednesday, January 4, 2017

MUUNGANO WA MAREKANI WAHARIBU KWA MAKUSUDI MIUNDOMBINU YA SYRIA

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kuwa muungano unaoongozwa na Marekani unabomoa kwa makusudi miundombinu ya Syria.
Igor Konashenkov ametoa taarifa Jumatano hii akieleza kuwa, muungano unaofanya mashambulizi dhidi ya Daesh chini ya uongozi wa Marekani kuanzia mwaka 2012 hadi sasa haujazishambulia ngome za kundi hilo, bali umebomoa na kuharibu kwa makusudi miundombinu ya Syria.
Mfano wa uharibifu uliofanywa huko Syria na ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani 
Konashenkov ameongeza kuwa John Brennan Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) anafahamu vyema ukweli huo; hii ni kwa sababu muda mrefu kabla ya kuanza oparesheni za kijeshi za Russia huko Syria, muungano huo unaoongozwa na Marekani ulibomoa miundombinu ya Syra kwa lengo la kuidhoofisha serikali halali ya nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitoa taarifa hiyo jana Jumatano kufuatia tuhuma zilizoelekezwa kwa Russia na mkuu wa CIA aliyesema kwamba Moscow inatekeleza siasa za kuangamiza mali na maliasili nchini Syria.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amebainisha kuwa, mashambulizi ya anga ya nchi hiyo huko Syria yameua maelfu ya magaidi; wakiwemo makamanda 204 wa magaidi hao katika medani za vita.
Itakumbukwa kuwa Russia ilianzisha mashambulizi ya anga huko Syria mwezi Septemba mwaka jana kufuatia ombi la Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad. 

No comments:

Post a Comment