Monday, January 2, 2017

GAMBIA YAFUNGA VITUO VIWILI VYA KATIKA MGOGORO WA BAADA YA UCHAGUZI


Maafisa wa usalama Gambia wamefunga vituo viwili vya radio binafsi karibu na mji mkuu Banjul huku nchi hiyo ikikumbwa na mgogoro wa baada ya uchaguzi.
Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Gambia ilisema jana kuwa, vituo vya redio vya Teranga FM na Hilltop Radio vilifungwa juzi Jumapili katika oparesheni iliyoendeshwa na maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa taifa. Serikali haijatoa taarifa yoyote kuhuhsiana na tukio hilo.
Mgogoro wa kisiasa Gambia uliibuka pale Rais Yahya Jammeh  ambaye kipindi chake cha kuweko madarakani kinamalizika tarehe 19 ya mwezi huu wa Januari, alipokataa matokeo ya uchaguzi ingawa awali alikuwa amekubali kushindwa, na hivyo kuzusha hofu ya uwezekano wa mataifa ya eneo la magharibi mwa Afrika kuingilia kati na kumuondoa madarakani kwa nguvu.

Adama Barrow
Katika hotuba yake hiyo ya mwaka mpya Rais wa Gambia amesema, azimio lililopitishwa na ECOWAS kwamba itatumia kila njia iwezekanayo kuhakikisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa Gambia yanaheshimiwa, ni kutangaza vita na kuivunjia heshima katiba ya nchi hiyo.
Jammeh ametangaza kuwa hatokabidhi madaraka; lakini rais mteule wa nchi hiyo Adama Barrow ametoa wito tena kwa kiongozi huyo kumtaka angátuke madarakani kwa njia za amani.

No comments:

Post a Comment