Monday, January 30, 2017

JESHI LA YEMEN LAANGAMIZA MELI YA MIZIGO YA SAUDIA, RIYADH YAKIRI

Jeshi la Yemen Jumatatu ya jana liliangamiza meli ya mizinga ya Saudia na kusababisha makumi ya askari wa nchi hiyo vamizi kuangamizwa na wengine kujeruhiwa.
Sambamba na Saudia kukiri juu ya habari hiyo imedai kuwa, katika shambulizi la jeshi la Yemen dhidi ya meli yake ya mizinga katika pwani ya mkoa wa Al Hudaydah, askari wake wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa. Wakati huo huo jeshi la Saudia limeshambulia mji mdogo wa pwani wa Al Mukha kusini mwa mkoa wa Taiz na kusababisha makumi ya raia kuuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa.
Mfalme wa Saudia anayetekeleza jinai na mauaji dhidi ya raia madhlumu wa Yemen
Aidha shambulizi hilo lilililenga daraja la Irfan mjini humo. Kwingineko jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah imeangamiza askari vibaraka wa Saudia waliokuwa wanakimbia uwanja wa mapigano baada ya kuzidiwa. Kwa mujibu wa habari hiyo askari kadhaa vibaraka wa Aal-Saud wameangamizwa katika mkoa wa Taiz kusini magharibi mwa Yemen.
Sehemu ya jinai za utawala wa kidikteta wa Aal-Saud huko Yemen
Hii ni katika hali ambayo kwa mara nyingine jeshi la Yemen limezilenga kambi za jeshi la Saudia za Jizan na kuisababisha nchi hiyo kibaraka wa Marekani na Israel hasara ya maafa na uharibifu. Kama ambavyo jeshi hilo la Yemen na harakati ya Answarullah limeshambulia kwa makombora mengi kambi ya jeshi ya al-Makhruq iliyopo eneo la Quwah mkoani Najran na kuangamiza askari kadhaa.

No comments:

Post a Comment