Tuesday, January 3, 2017

MWENYEKITI WA TUME YAUCHAGUZI NCHINI GAMBIA AKIMBILIA MAFICHONI

media
Alieu Momar Njai, 

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Gambia, Alieu Momar Njai, ameondoka nchini, kwa mujibu wa ripoti kadhaa. Familia yake imefahamisha BBC kuwa hayupo nchini Gambia, na kamwe haitofichua eneo ambapo amekimbilia .
Inaarifiwa kuwa Alieu Momar Njai alikimbilia mafichoni kufuatia vitisho vya kuuawa baada ya kutangazwa kushindwa kwa Yahya Jammeh katika uchaguzi wa urais.
Rais anayemaliza muda wake kwa mara ya kwanza alikubali kushindwa na kupongeza ushindi wa mpinzani wake Adama Barrow, lakini baadae alipinga ushindi huo na kuitaka mahakam kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais, akisema uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.
Tume ya Uchaguzi ilitangaza kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Kufunguliwa upya kwa ofisi za Tume ya Uchaguzi
Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yalifunguliwa wiki iliyopita kwa uamuzi wa serikali ya Gambia.
Desemba 13, makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yalifungwa na kuzingirwa na vikosi vya usalama, kutokana na hatari ya kuchomwa moto, serikali imetangaza. Serikali imeongeza kuwa "vikosi vya usalama vitasalia katika hilo.

No comments:

Post a Comment