Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza
kwamba Jamhuri ya Kiislamu itayawasilisha Umoja wa Mataifa madai ya
Nikki Haley, balozi wa Marekani katika umoja huo kwamba eti Iran
imeipatia silaha harakati ya Ansarullah ya Yemen.
Katika ujumbe wa baruapepe aliotuma kwa shirika la habari la
Russia la Sputnik, Dakta Zarif ameandika: Jamhuri ya Kiislamu
itawasilisha malalamiko Umoja wa Mataifa dhidi ya madai yaliyotolewa na
Marekani.
Siku ya Alkhamisi iliyopita, huku akiwa amesimama kando ya mabaki
kadhaa ya vyuma, Haley alianzisha propaganda mpya dhidi ya Iran kwa
kudai kwamba vyuma hivyo ni mabaki ya makombora ya Iran.
Pasi na kuashiria misaada ya silaha inayotolewa na Marekani kwa Saudi
Arabia, silaha ambazo zinatumika kuwashambulia raia madhulumu wa Yemen,
Haley aliituhumu Iran kuwa eti inaizatiti kwa silaha harakati ya
Ansarullah ya Yemen kwa ajili ya kuishambulia kwa makombora Saudia.
Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq ameyakanusha madai hayo yaliyotolewa na balozi wa Marekani katika umoja huo.
Kwa msaada na uungaji mkono wa Marekani, tangu mwezi Machi mwaka 2015
Saudi Arabia imeanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen na kuiwekea
nchi hiyo mzingiro wa ardhini, baharini na angani. Moto wa vita
uliowashwa na Saudia na waitifaki wake hadi sasa umesababisha makumi ya
maelfu ya watu kuuawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wengine kubaki bila
makaazi.
Muungano huo vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud
umekuwa kila mara ukidai kwamba Iran inavipatia vikosi vya wananchi wa
Yemen silaha na makombora na kwamba eti kwa kufanya hivyo inakwamisha
utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo.
Hata hivyo viongozi wa Yemen wamesisitiza mara kadhaa kuwa uwezo wa
kiulinzi na wa kujihami wa jeshi la nchi hiyo unatokana na nguvu zake za
ndani na kwamba licha ya mzingiro wa kila upande uliowekwa na utawala
wa Aal Saud, uwezo huo unaongezeka siku baada ya siku.
Utawala wa Aal Saud na Marekani hadi sasa zimeshindwa kufikia malengo
yao nchini Yemen ya kuwaweka vibaraka wao madarakani kutokana na
muqawama wa wananchi wa nchi hiyo.../
No comments:
Post a Comment