Wananchi wa Mauritania wameungana na Waislamu
na wapenda haki katika kona zote za dunia kuendeleza maandamano ya
kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa hatua yake ya kuitambua Quds
kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
Mtandao wa gazeti la al Quds al
Arabi umetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, maeneo mbalimbali ya
Mauritania yameendelea kushuhudia maandamano ya kupinga uamuzi wa Trump
kuhusiana na mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas huku maelfu ya watu
walioshiriki kwenye maandamano hayo wakitoa nara za "Mauti kwa
Marekani," "Quds ni Yetu," "Mtake Msitake, Quds ni Mji Mkuu wa
Palestina" na "Hatutoruhusu Kuporwa Quds."
Watu wa matabaka mbalimbali nchini
Mauritania wametoa matamko wakiitaka serikali ya nchi hiyo na nchi
nyingine za Kiarabu na Kiislamu kukata uhusiano wao na Marekani kama
njia ya kupinga uamuzi wa Donald Trump wa kuitambua rasmi Baytul
Muqaddas kuwa kuwa eti ni mji mkuu wa Israel.
Donald Trump alitumia hotuba yake ya
siku ya Jumatano kufanya uchokozi wa wazi kwa kuitangaza Quds ambayo ina
Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa
Kizayuni na hapo hapo akatoa amri ya kuanza mchakato wa kuhamishiwa
Baytul Muqaddas, ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv, mji mkuu wa
utawala wa Kizayuni.
Viongozi wa nchi mbalimbali duniani nao
wamelaani hatua hiyo wakiwemo wa Ulaya kama Uingereza na Papa Francis,
kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani. Hata Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea
Kaskazini ameubeza uamuzi huo wa rais wa Marekani wa kuitangaza Quds
kuwa mji mkuu wa Israel na kusema kuwa, hakuna nchi inayoitwa Israel
hata Baitul Muqaddas uwe mji mkuu wake.
No comments:
Post a Comment