Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye
Umoja wa Mataifa amesema amestaajabishwa sana na kitendo cha jeshi la
Israel kumuua kwa kumpiga risasi mtu mwenye ulemavu aliyekuwa anaelekea
msikitini siku ya Ijumaa.
Zeid Ra'ad Al Hussein Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye
Umoja wa Mataifa ametoa kauli hiyo kufuatia ripoti kwamba mtu huyo
Ibrahim Abu Thurayeh aliuawa shahidi akiwa kwenye kitimwendo chake.
Ibrahim alikuwa miongoni mwa mamia ya Wapalestina walioandamana
Ijumaa karibu na uzio kati ya Ukanda wa Gaza na Israel, wakipinga hatua
ya Marekani kutambua mji wa Quds (Jerusalem) kuwa eti ni mji mkuu wa
utawala bandia wa Israel.
Zeid amesema taarifa zinadhihirisha kuwa jeshi la Israel lilitumia
nguvu nyingi kupita kiasi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za
kimataifa za kibinadamu.
Hili ni janga la pili kumkuta Ibrahim ambapo mwaka 2008 makombora yaliyorushwa na Israel yalimkataa miguu yake miwili.
Afisa huyo wa Umoja wa Maaifa ametaka hatua za kisheria zichuliwe dhidi ya waliotekeza jinai hiyo.
No comments:
Post a Comment