Hata askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshindwa kuzima uasi nchini Mali
Duru za kiusalama za Mali zimetangaza kuwa
watu sita wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi
lililofanywa na watu wenye silaha katika mji wa Timbuktu wa kaskazini
mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Duru hizo zimesema, baadhi ya watu waliouawa ni wanachama wa kundi linalojulikana kwa jina la Tawariq.
Watu hao wameuawa baada ya gari lao
kushambuliwa na watu wenye silaha ambapo mbali na kuuawa watu sita na
kujeruhiwa wengine watatu, watu wengine wawili waliokuwemo kwenye gari
hiyo hadi hivi sasa hawajulikani waliko.
Nchi ya Mali ilikumbwa na machafuko tangu mwaka 2012 wakati
yalipotokea mapinduzi ya kijeshi na hapo hapo ukazuka uasi kaskazini mwa
nchi hiyo uliopelekea kutekwa na waasi, eneo kubwa la nchi hiyo.
Askari wa Umoja wa Mataifa pamoja na
wale wa mkoloni Ufaransa walitumwa nchini Mali katikati ya mwaka 2013,
lakini pamoja na hayo wameshindwa kuzima uasi huo licha ya kukomboa
baadhi ya maeneo yaliyokuwa yametekwa.
Licha ya kutiwa saini makubaliano ya
amani baina ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha ya kaskaizni mwa
nchi hiyo mwaka 2015, lakini machafuko bado yanaendelea huku mauaji ya
mara kwa mara na mashambulizi ya kushitukiza yakiripotiwa katika maeneo
tofauti ya kaskazini mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment