Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Kenya, Raila Odinga.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga amesema ataapishwa kama rais wa watu mapema mwaka 2018.
Katika ujumbe wake wa Krismasi, Odinga
ameonya kuwa Kenya inaelekea kuwa taifa la Kidikteta na kuwataka wafuasi
wake kuendelea kuunga mkono mikakati ya upinzani.
Serikali imeonya kuwa Odinga
atafunguliwa mashtaka ya uhaini iwapo ataapishwa, onyo ambalo kiongozi
huyo wa NASA amesema yuko tayari kukabiliana nalo ikiwa ndio itakuwa
njia ya kuleta haki ya kisiasa katika taifa hilo.
Iwapo Odinga, atatekeleza mipango yake,
itaendeleza kuzua mvutano wa kisiasa katika taifa hilo ambalo limemaliza
Uchaguzi hivi karibuni.
Marekani imetaka kuwepo kwa mazungumzo
kati ya Odinga na Kenyatta, na kumhimiza kiongozi huyo wa NASA
kutojiapisha kwa kile inachosema kitendo hicho kitaendelea kuzua mzozo
wa kisiasa.
Kenyatta amenukuliwa mara kadhaa akisema
kuwa, yuko tayari kuzungumza na Odinga lakini mazungumzo hayo yawe ni
kuhusu maendeleo ya nchi huku Odinga akisema atashiriki tu kuhusu
mazungumzo yatakayokuwa na ajenda ya namna ya kuwa na Uchaguzi wa urais
utakaokuwa huru na haki.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment