Wanawake wanaomtuhumu Rais Donald Trump wa
Marekani kwamba aliwanyanyasa kingono wamelitaka Bunge la nchi hiyo
(Kongresi) kufanya uchunguzi kuhusu kashfa za kimaadili za kiongozi
huyo.
Wanawake hao wanaosema walinyanyaswa kijinsia na Trump
walitarajiwa kukutana leo kwa mara ya kwanza na kutoa wito wa kuanza
uchunguzi kuhusu kashfa za kingono za Donald Trump.
Wakati
huo huo balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley amesema
kuwa wanawake wanaomtuhumu Rais Donald Trump kuwa aliwanyanyasa
kijinsia wanapaswa kuzikilizwa.
Haley amesema wanawake hao wanapaswa kusikilizwa na kesi yao inapaswa kushughulikiwa.
Gavana
huyo wa zamani na mmoja kati ya wanawake wenye vyeo vya juu katika
utawala wa Trump, amesema wakati umefika wa kutafakari kwa kina kuhusu
jinsi wanawake wanavyotendewa nchini Marekani.
Matamshi hayo ya balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
yanakwenda kinyume kabisa na sisitizo la serikali ya nchi hiyo ambayo
imekuwa ikidai kuwa kashfa za kuwanyanyasa kijinsia wanawake
zinazomkabili Donald Trump hazina msingi.
Makumi
ya wanawake wamemtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kuwa
aliwanyanyasa kingono ikiwa ni pamoja na kuwapapasa papasa, kuwabusu kwa
kuwalazimisha na kutumia maneno machafu na ya utovu wa maadili.
No comments:
Post a Comment