Chama cha Kizayuni cha Likud kimewataka
viongozi na wawakilishi wa Bunge la utawala haramu la Israel kuhudhuria
kikao cha dharura cha chama kwa ajili ya kuchunguza uamuzi wa
kudhibitiwa kikamilifu na utawala huo, eneo la Ukingo wa Magharibi wa
Mto Jordan huko Palestina.
Televisheni namba mbili ya Israel
imetangaza kwamba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho,
maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na kikao hicho, yatatakiwa kutekelezwa
na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel ambapo kwanza atatakiwa
kuyawasilisha katika Bunge la utawala huo (Knesset) kwa ajili ya
kupasishwa.
Aidha televisheni ya Israel imetangaza
kuwa, lengo la kikao hicho ni kupasisha sheria ya kuliunganisha eneo la
Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na
Israel. Taarifa hiyo imedai kwamba, harakati hiyo ilianza tangu Rais
Donald Trump wa Marekani alipoutangaza mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji
mkuu wa Israel sambamba na kutaka kuanzishwa maandalizi kwa ajili ya
kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo kwenda mji huo.
No comments:
Post a Comment