Televisheni ya al Masirah imetangaza kuwa
watu wasiopungua 15 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga ya Saudi
Arabia katika maeneo mbalimbali huko Yemen, ukiwemo mji mkuu Sana'a.
Ndege
za kivita za Saudi Arabia mapema leo zimeyashambulia mashamba mawili
katika wilaya ya Zabid katika mkoa wa Hudaydah na kuua watu wanane
wakiwemo wanawake wawili. Wanawake wengine wawili wamejeruhiwa pia
katika mashambulizi hayo.
Ndege hizo za kivita za Saudia leo pia
zilifanya mashambulizi kadhaa katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kuua
raia saba na kujeruhi wengine watano. Watoto watatu na wanawake wawili
ni miongoni mwa raia waliojeruhiwa huko Sana'a huku watu wengine wawili
wakiwa hawajulikani walipo. Televisheni ya al Masirah imeripoti kuwa
nyumba moja iliyolengwa na ndege za kivita za Saudi Arabia katika mji
mkuu Sana'a imeharibiwa kikamilifu na kwamba wafanyakazi wa huduma za
uokoaji waliokuwa wakiwatafuta majeruhi waliofunikwa na vifusi vya
nyumba hiyo nao pia wamelengwa na ndege hizo za kivita za Saudia. Watu
walioshuhudia wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye mashambulizi
hayo ya Saudia huenda ikaongezeka.
No comments:
Post a Comment