Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
zimekubaliana kuimarisha utaratibu wa mawasiliano na kupeana taarifa za
kiintelijensia kwa ajili ya kupambana na waasi wa ADF kufuatia
mashambulizi yao dhidi ya vikosi vya walinzi wa amani wa Umoja wa
Mataifa.
Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia
Richard Karemire amesema serikali ya Uganda na maofisa wa Kivu ya
Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa na mkutano wa
usalama.
Msemaji
huyo amesema kupeana taarifa kutasaidia vikosi vijiandae kuwazuia waasi
kujipenyeza ndani na mashambulizi yanayoweza kufanywa na ADF.
Hivi karibuni askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliuawa , 44 walijeruhiwa na wengine wawili hawajulikani walipo kufuatia hujuma ya waasi wa ADF.
Tukio hilo lilitokea Desemba 7,2017
katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini
mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu.
Askari waliouawa walikuwa ni sehemu
ya askari 3,000 wa tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa MONUSCO
yenye askari kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment