Mjumbe wa ngazi ya juu wa Harakati ya
Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo inatekeleza
njama za kumuua shahidi Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa harakati
hiyo.
Ibrahim Suleiman ameashiria
pingamizi la kila mara la serikali ya Nigeria kuhusiana na takwa
la familia ya Sheikh Zakzaky la kumpeleka nje ya nchi kiongozi huyo wa
Kiislamu kwa ajili ya matibabu licha ya hali ya mwanazuoni huyo kuwa
mbaya. Mwakilishi huyo wa ngazi ya juu wa Harakati ya Kiislamu ya
Nigeria ameongeza kuwa upo uwezekano kuwa njama zinafanywa ili kumuua
shahidi pole pole Sheikh Zakzaky. Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na mkewe walitiwa mbaroni katika
shambulizi lililofanywa Disemba 13 mwaka juzi na wanajeshi wa Nigeria
katika Husseiniya iliyopo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini
mwa nchi hiyo. Mamia ya waumini wa Kiislamu wakiwemo watoto watatu wa
Sheikh Zakzaky waliuliwa shahidi katika tukio hilo.
Hassan al-Banna, mjumbe wa Harakati ya
Kiislamu ya Nigeria sambamba na kuashiria mashtaka ya harakati
hiyo dhidi ya serikali ya Nigeria katika Umoja wa Afrika amesema kuwa,
licha ya kutolewa amri ya mahakama ya kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky
pamoja na mkewe, lakini serikali ya Abuja imekataa katakata kutekeleza
amri hiyo. Kwa muda sasa serikali imekuwa ikitekeleza siasa za chuki na
adawa dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Kutiwa mbaroni Sheikh Ibrahim Zakzaky na kushadidi mashinikizo dhidi
ya Waislamu sambamba na kupigwa marufuku mkusanyiko wa aina yoyote ile
wa Waislamu wa nchi hiyo ni miongoni mwa siasa ambazo zimekuwa
zikitekelezwa na serikali ya Rais Muhammadu Buhari dhidi ya Waislamu wa
Nigeria.
Hatua hizo zinatekelezwa katika hali
ambayo, hivi karibuni Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty
International sambamba na kutahadharisha kuhusiana na kutoweka idadi
kadhaa ya Waislamu wa Nigeria, lilikosoa vikali utendaji wa serikali ya
Abuja katika uwanja huo na kuitaka serikali hiyo ianzishe
uchunguzi kuhusiana na kutoweka wanachama 600 wa Harakati hiyo ya
Kishia.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa,
serikali ya Nigeria inachukua hatua hizo chini ya ushawishi wa siasa za
utawala wa Saudia, Marekani na utawala dhalimu wa Israel. Ni kwa muda
sasa ambapo Wazayuni baada ya siasa zao kugonga mwamba katika eneo la
Mashariki ya Kati na kutengwa, sasa wameligeukia bara la Afrika na wamo
mbioni kutafuta washirika wao wapya katika bara hilo.
Katika fremu hiyo, hivi karibuni baadhi ya makamanda wa jeshi la
Nigeria walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kijeshi wa
utawala wa Kizayuni wa Israel. Saudia ni nchi nyingine ambayo imekuwa
ikihaha kuhakikisha kuwa inakuwa na satuwa na ushawishi barani Afrika.
Misaada ya siri na dhahiri ya kifedha na
kijeshi ya Saudia kwa nchi za bara hilo na mkabala wake nchi hizo
zisalimu amri mbele ya matakwa ya utawala wa Riyadh ni baadhi ya
mikakati inayofanywa na watawala wa Aal Saud. Marekani nayo kwa kuiuzia
silaha na zana za kijeshi serikali ya Nigeria imekuwa ikisaidia katika
kukandamizwa Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Katika uga
huo, hivi karibuni Abdul-Rahman Abubakar Mkuu wa Kamati ya
Kufuatilia Kuachiliwa Huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, sanjari na kuitumia
barua serikali ya Marekani na kuashiria rekodi ambayo haijawahi
kushuhudiwa ya serikali ya Nigeria kukiuka na kukandamiza haki za
binadamu, ameitaka Washington iache kuiuzia silaha nchi hiyo.
Filihali kwa kuzingatia uadui wa tawala
tatu za Israel, Saudia na Marekani dhidi ya harakati za kupigania uhuru
za Kiislamu na ushawishi wa tawala hizo nchini Nigeria, suala la hatari
ya kuuawa shahidi Sheikh Ibrahim Zakzaky na setikali ya Nigeria kufanya
hilo kwa makusudi ni jambo ambalo linazidi kupata nguvu
No comments:
Post a Comment