China imezindua ndege ya "Jiaolong" AG600 ambayo ni ndege kubwa zaidi duniani inayoweza kutua nchi kavu na majini.
Ndege hiyo imeundwa kikamilifu
nchini China na jana ilifanikiwa kuruka kwa majaribio. Ndege hiyo ni kwa
ajili ya kukabiliana na ajali za moto misituni, na uokoaji watu majini.
Inaweza kuvuta maji tani 20 ndani ya sekunde 20, na kuzima moto katika
eneo la mita za mraba zaidi ya 4,000 mara moja, huku ikiweza kuwaokoa
watu 50 baharini mara moja. Mbali na kuzima moto na kuwaokoa watu, pia
inaweza kutumiwa katika uchunguzi na uhifadhi wa mazingira baharini.
Ndege hiyo pia inaweza kutumika kijeshi
na inatathminiwa kuwa uzinduzi wake ni katika jitiahda za China za
kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi.
Mapema mwaka huu, China ilizindua meli yake ya kwanza ya kivita yenye kusheheni ndege (aircraft carrier) iliyoundwa nchini humo.
No comments:
Post a Comment