Rais wa Guatemala Jimmy Morales ameamrisha ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel kuhamishwa kwenda Jurusalen.
Katika
ujumbe kupitia Facebook, Bw. Morales alisema kuwa hatua hiyo
ilichukuliwa baada ya kuzungumza na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
Wiki
iliyopita Guatemala ilikuwa moja ya nchi tisa zilizopiga kura kupinga
azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta hatua ya kuitambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Donald Trump alitishia kupunguza misaada kwa nchi ambazo zilipiga kura dhidi ya Marekani.
- Trump: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel
- Trump awatishia watakaounga mkono maazimio ya UN juu ya mji wa Jerusalem
Marekani ni mtoaji muhimu wa misaada kwa Guatemala, nchi maskini ya kati kati mwa Amerika.
Siku
ya Jumapili Bw. Morales alisema kuwa alikuwa ameamrisha mmlaka za nchi
hiyo kufanya mikakati ya kuhamisha ubalozi kutoka Tel Aviv kwenda
Jerusalem.
Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestiona.
Israel
ilitwaa mji huo ambao awali ulikuwa ukikaliwa na Jordan wakati wa vita
vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati na inaitaja mji wote huo kuwa mji
wake mkuu.
Wapalestina wanadai kuwa East Jerusalem ni mji wao mkuu taifa lake la baadaye.
Jerusalem haujatambuliwa kimataifa na nchi zote kwa sasa zina balozi zao huko Tel Aviv.
No comments:
Post a Comment