Korea Kaskazini imeapa kufanyia majaribio
zaidi ya zana zake za nyuklia mwaka 2018 huku ikisisitiza kuwa uwezo
wake hauwezi kuangamizwa au kuvurugwa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyosambazwa kupitia shirika rasmi la habari la
Korea Kaskazini KCNA, wakuu wa Korea Kaskazini wameilamu Marekani kwa
kuendeleza njama dhidi yake katika sekta za kiuchumi, kisiasa, kijeshi
na kidiplomasia katika mwaka huu unaomalizika wa 2017. Taarifa hiyo
imesema pamoja na kuwepo njama hizo za Marekani Korea Kaskazini
haikusita katika mkondo wake na ina yakini ya kupata ushindi.
Aidha
Korea Kaskazini imesema itazidi kuimarisha uwezo wake wa kujihami ili
kukabiliana na vitisho vya nyuklia vya Marekani. Wakuu wa Pyongyang pia
wameilaumu vikali Marekani kwa kuendeleza uchochezi kupitia vitisho vya
nyuklia na mazoezi ya kijeshi katika mipaka yake.
Septemba mwaka huu, Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kwa mafanikio
bomu la nyuklia, hilo likiwa ni jaribio la sita la aina hii kufanywa na
nchi hiyo.
Marekani,
ambayo ni mchochezi mkuu wa mivutano kwenye eneo la Peninsula ya Korea
imekuwa kila mara ikishikilia Korea Kaskazini isimamishe majaribio yake
ya nyuklia, lakini viongozi wa Pyongyang wanasisitiza kwamba madamu
Marekani na waitifaki wake wanaendelea kutoa vitisho dhidi ya Korea
Kaskazini, nchi hiyo nayo itaendelea kujiimarisha kijeshi.
Jeshi la Uganda limetangaza habari ya kuua
wanachama wasiopungua 100 wa kundi la waasi wa ADF katika makabiliano
makali yaliyojiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa iliyotolewa jana Jumatano na Jeshi la Ulinzi la Uganda
UPDF imesema kuwa, vikosi vyake vimefanya mashambulizi ya angani na
ardhini dhidi ya maficho ya waasi hao katika mpaka wa nchi hiyo ya
Afrika Mashariki na Kongo DR, na kufanikiwa kuua zaidi ya 100 miongoni
mwao na kujeruhi wengine wengi.
Hujuma hii dhidi ya waasi wa ADF imefanyika siku chache baada
ya Uganda na Kongo DR kukubaliana kuimarisha utaratibu wa mawasiliano na
kupeana taarifa za kiintelijensia kwa ajili ya kupambana na waasi hao
wanaotokea Uganda, ambao wanaendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
Itakumbukwa kuwa, askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
waliuawa mwanzoni mwa mwezi huu wa Disemba, na 44 wengine walijeruhiwa
katika kambi ya Semuliki mkoani Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia hujuma ya waasi hao wa ADF.
Wanajeshi waliouawa walikuwa ni sehemu ya askari 3,000 wa timu ya
kulinda amani ya Umoja wa Mataifa MONUSCO yenye askari kutoka Tanzania,
Malawi na Afrika Kusini.
Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Kenya, Raila Odinga.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga amesema ataapishwa kama rais wa watu mapema mwaka 2018.
Katika ujumbe wake wa Krismasi, Odinga
ameonya kuwa Kenya inaelekea kuwa taifa la Kidikteta na kuwataka wafuasi
wake kuendelea kuunga mkono mikakati ya upinzani.
Serikali imeonya kuwa Odinga
atafunguliwa mashtaka ya uhaini iwapo ataapishwa, onyo ambalo kiongozi
huyo wa NASA amesema yuko tayari kukabiliana nalo ikiwa ndio itakuwa
njia ya kuleta haki ya kisiasa katika taifa hilo.
Iwapo Odinga, atatekeleza mipango yake,
itaendeleza kuzua mvutano wa kisiasa katika taifa hilo ambalo limemaliza
Uchaguzi hivi karibuni.
Marekani imetaka kuwepo kwa mazungumzo
kati ya Odinga na Kenyatta, na kumhimiza kiongozi huyo wa NASA
kutojiapisha kwa kile inachosema kitendo hicho kitaendelea kuzua mzozo
wa kisiasa.
Kenyatta amenukuliwa mara kadhaa akisema
kuwa, yuko tayari kuzungumza na Odinga lakini mazungumzo hayo yawe ni
kuhusu maendeleo ya nchi huku Odinga akisema atashiriki tu kuhusu
mazungumzo yatakayokuwa na ajenda ya namna ya kuwa na Uchaguzi wa urais
utakaokuwa huru na haki.
Chama cha Kizayuni cha Likud kimewataka
viongozi na wawakilishi wa Bunge la utawala haramu la Israel kuhudhuria
kikao cha dharura cha chama kwa ajili ya kuchunguza uamuzi wa
kudhibitiwa kikamilifu na utawala huo, eneo la Ukingo wa Magharibi wa
Mto Jordan huko Palestina.
Televisheni namba mbili ya Israel
imetangaza kwamba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho,
maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na kikao hicho, yatatakiwa kutekelezwa
na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel ambapo kwanza atatakiwa
kuyawasilisha katika Bunge la utawala huo (Knesset) kwa ajili ya
kupasishwa.
Aidha televisheni ya Israel imetangaza
kuwa, lengo la kikao hicho ni kupasisha sheria ya kuliunganisha eneo la
Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na
Israel. Taarifa hiyo imedai kwamba, harakati hiyo ilianza tangu Rais
Donald Trump wa Marekani alipoutangaza mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji
mkuu wa Israel sambamba na kutaka kuanzishwa maandalizi kwa ajili ya
kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo kwenda mji huo.
Mjumbe wa ngazi ya juu wa Harakati ya
Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo inatekeleza
njama za kumuua shahidi Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa harakati
hiyo.
Ibrahim Suleiman ameashiria
pingamizi la kila mara la serikali ya Nigeria kuhusiana na takwa
la familia ya Sheikh Zakzaky la kumpeleka nje ya nchi kiongozi huyo wa
Kiislamu kwa ajili ya matibabu licha ya hali ya mwanazuoni huyo kuwa
mbaya. Mwakilishi huyo wa ngazi ya juu wa Harakati ya Kiislamu ya
Nigeria ameongeza kuwa upo uwezekano kuwa njama zinafanywa ili kumuua
shahidi pole pole Sheikh Zakzaky. Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na mkewe walitiwa mbaroni katika
shambulizi lililofanywa Disemba 13 mwaka juzi na wanajeshi wa Nigeria
katika Husseiniya iliyopo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini
mwa nchi hiyo. Mamia ya waumini wa Kiislamu wakiwemo watoto watatu wa
Sheikh Zakzaky waliuliwa shahidi katika tukio hilo.
Hassan al-Banna, mjumbe wa Harakati ya
Kiislamu ya Nigeria sambamba na kuashiria mashtaka ya harakati
hiyo dhidi ya serikali ya Nigeria katika Umoja wa Afrika amesema kuwa,
licha ya kutolewa amri ya mahakama ya kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky
pamoja na mkewe, lakini serikali ya Abuja imekataa katakata kutekeleza
amri hiyo. Kwa muda sasa serikali imekuwa ikitekeleza siasa za chuki na
adawa dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Kutiwa mbaroni Sheikh Ibrahim Zakzaky na kushadidi mashinikizo dhidi
ya Waislamu sambamba na kupigwa marufuku mkusanyiko wa aina yoyote ile
wa Waislamu wa nchi hiyo ni miongoni mwa siasa ambazo zimekuwa
zikitekelezwa na serikali ya Rais Muhammadu Buhari dhidi ya Waislamu wa
Nigeria.
Hatua hizo zinatekelezwa katika hali
ambayo, hivi karibuni Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty
International sambamba na kutahadharisha kuhusiana na kutoweka idadi
kadhaa ya Waislamu wa Nigeria, lilikosoa vikali utendaji wa serikali ya
Abuja katika uwanja huo na kuitaka serikali hiyo ianzishe
uchunguzi kuhusiana na kutoweka wanachama 600 wa Harakati hiyo ya
Kishia.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa,
serikali ya Nigeria inachukua hatua hizo chini ya ushawishi wa siasa za
utawala wa Saudia, Marekani na utawala dhalimu wa Israel. Ni kwa muda
sasa ambapo Wazayuni baada ya siasa zao kugonga mwamba katika eneo la
Mashariki ya Kati na kutengwa, sasa wameligeukia bara la Afrika na wamo
mbioni kutafuta washirika wao wapya katika bara hilo.
Katika fremu hiyo, hivi karibuni baadhi ya makamanda wa jeshi la
Nigeria walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kijeshi wa
utawala wa Kizayuni wa Israel. Saudia ni nchi nyingine ambayo imekuwa
ikihaha kuhakikisha kuwa inakuwa na satuwa na ushawishi barani Afrika.
Misaada ya siri na dhahiri ya kifedha na
kijeshi ya Saudia kwa nchi za bara hilo na mkabala wake nchi hizo
zisalimu amri mbele ya matakwa ya utawala wa Riyadh ni baadhi ya
mikakati inayofanywa na watawala wa Aal Saud. Marekani nayo kwa kuiuzia
silaha na zana za kijeshi serikali ya Nigeria imekuwa ikisaidia katika
kukandamizwa Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Katika uga
huo, hivi karibuni Abdul-Rahman Abubakar Mkuu wa Kamati ya
Kufuatilia Kuachiliwa Huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, sanjari na kuitumia
barua serikali ya Marekani na kuashiria rekodi ambayo haijawahi
kushuhudiwa ya serikali ya Nigeria kukiuka na kukandamiza haki za
binadamu, ameitaka Washington iache kuiuzia silaha nchi hiyo.
Filihali kwa kuzingatia uadui wa tawala
tatu za Israel, Saudia na Marekani dhidi ya harakati za kupigania uhuru
za Kiislamu na ushawishi wa tawala hizo nchini Nigeria, suala la hatari
ya kuuawa shahidi Sheikh Ibrahim Zakzaky na setikali ya Nigeria kufanya
hilo kwa makusudi ni jambo ambalo linazidi kupata nguvu
Televisheni ya al Masirah imetangaza kuwa
watu wasiopungua 15 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga ya Saudi
Arabia katika maeneo mbalimbali huko Yemen, ukiwemo mji mkuu Sana'a.
Ndege
za kivita za Saudi Arabia mapema leo zimeyashambulia mashamba mawili
katika wilaya ya Zabid katika mkoa wa Hudaydah na kuua watu wanane
wakiwemo wanawake wawili. Wanawake wengine wawili wamejeruhiwa pia
katika mashambulizi hayo.
Ndege hizo za kivita za Saudia leo pia
zilifanya mashambulizi kadhaa katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kuua
raia saba na kujeruhi wengine watano. Watoto watatu na wanawake wawili
ni miongoni mwa raia waliojeruhiwa huko Sana'a huku watu wengine wawili
wakiwa hawajulikani walipo. Televisheni ya al Masirah imeripoti kuwa
nyumba moja iliyolengwa na ndege za kivita za Saudi Arabia katika mji
mkuu Sana'a imeharibiwa kikamilifu na kwamba wafanyakazi wa huduma za
uokoaji waliokuwa wakiwatafuta majeruhi waliofunikwa na vifusi vya
nyumba hiyo nao pia wamelengwa na ndege hizo za kivita za Saudia. Watu
walioshuhudia wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye mashambulizi
hayo ya Saudia huenda ikaongezeka.
Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ya Bahrain
imelaani hukumu iliyotolewa na mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo kwa raia
wa nchi hiyo na kuitaja kuwa ni batili.
Jumuiya hiyo imesisitiza leo
ikijibu hatua ya mahakama kuu ya kijeshi ya Bahrain ya kuwakatia hukumu
ya kifo raia wa nchi hiyo kwamba kutishiwa kuuawa, kulazimishwa kukiri
chini ya mateso kama kuadhibiwa kwa kushtushwa na umeme, kutishia
kuwabaka ndugu na familia, kutekwa na kutiwa mbaroni kwa kificho kuwa ni
vitendo visivyo vya kibinadamu wanavyofanyiwa raia wa Bahrain.
Taaarifa ya Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq imeongeza kuwa jamii ya
kimataifa inapasa kuvunja kimya chake na kujiondoa katika kifungo cha
wenzo wa mashinikizo wa mafuta na dola, na badala yake ionyeshe msimamo
na ichukue hatua mkabala na maafa na jinai hizo zinazojiri huko Bahrain
chini ya kivuli cha kukosekana uadilifu.
Jumuiya ya al Wifaq imesisitiza kuwa
fikra za ulipizaji kisasi haziwezi kudhibiti irada ya wananchi na kwamba
vyombo vya mahakama vinawanyima wananchi wa Bahrain haki zao za msingi
huku mahakama za kijeshi na vyombo vya usalama vikigeuzwa na kutumiwa
kama wenzo na utawala ulioko madarakani katika kuwatesa raia wanaopinga
utawala wa kidikteta na wa kifisadi wa nchi hiyo. Mahakama ya kijeshi ya
Bahrain leo Jumatatu imewahukumu kunyongwa raia sita wengine wa nchi
hiyo kwa tuhuma zisizo na msingi kwamba walihusika katika kupanga njama
ya kumuuwa Sheikh Khalifa bin Ahmed Al Khalifah kamanda mkuu wa jeshi la
nchi hiyo na vitendo vingine vya kigaidi.
Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya
Iran leo wamepitisha mpango wa dharura wa kuunga mkono Mapinduzi ya
Kiislamu ya watu wa Palestina na kusisitiza kwamba Baitul Muqaddas
utakuwa mji mkuu wa kudumu wa nchi ya Palestina.
Mpango huo wa dharura umepitishwa kwa kura 187 za ndiyo, 15 za
hapana huku wabunge tisa kati ya wabunge wote 233 waliohudhuria kikao
hicho cha wazi cha bunge la Iran wakiamua kutopiga kura.
Mpango huo uliopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
unaunganishwa kwenye Ibara nambari moja ya sheria ya kuunga mkono
Mapinduzi ya Kiislamu ya watu wa Palestina.
Mpango huo utawasilishwa kwenye kamati husika ya Majlisi ya Ushauri
ya Kiislamu na kuwekwa kwenye ajenda za kujadiliwa na kupitishwa rasmi
na bunge hilo ndani ya muda wa masaa 48 yajayo.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono thabiti wa mapambano ya
Wapalestina na imekuwa ikitoa wito kwa Waislamu wote duniani kuungana
dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel ambao Tehran haiutambui
asilani kuwa ni moja ya nchi za ulimwengu.
Itakumbukwa kuwa tarehe 6 Desemba, Rais Donald Trump wa Marekani
aliamsha hasira za walimwengu kwa kutangaza kuitambua Baitul Muqaddas
kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kuagiza zichukuliwe hatua
za maandalizi ya kuuhamishia katika mji huo ubalozi wa Marekani ulioko
Tel Aviv.
Hata hivyo siku ya Alkhamisi iliyopita, Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa lilipitisha azimio kwa wingi mkubwa wa kura 128 za 'ndiyo' dhidi
ya 9 tu za 'la' kupinga tangazo hilo la rais wa Marekani na kumtaka
abadilishe uamuzi wake huo.
Kwa mujibu wa azimio hilo, Umoja wa Mataifa hautoitambua Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.../
Rais wa Guatemala Jimmy Morales ameamrisha ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel kuhamishwa kwenda Jurusalen.
Katika
ujumbe kupitia Facebook, Bw. Morales alisema kuwa hatua hiyo
ilichukuliwa baada ya kuzungumza na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
Wiki
iliyopita Guatemala ilikuwa moja ya nchi tisa zilizopiga kura kupinga
azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta hatua ya kuitambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Donald Trump alitishia kupunguza misaada kwa nchi ambazo zilipiga kura dhidi ya Marekani.
Marekani ni mtoaji muhimu wa misaada kwa Guatemala, nchi maskini ya kati kati mwa Amerika.
Siku
ya Jumapili Bw. Morales alisema kuwa alikuwa ameamrisha mmlaka za nchi
hiyo kufanya mikakati ya kuhamisha ubalozi kutoka Tel Aviv kwenda
Jerusalem.
Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestiona.
Israel
ilitwaa mji huo ambao awali ulikuwa ukikaliwa na Jordan wakati wa vita
vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati na inaitaja mji wote huo kuwa mji
wake mkuu.
Kundi la kigaidi la ISIS limedai kuhusika na
hujuma ya kigaidi iliyolenga Idara ya Usalama wa Taifa ya Afghanistan
katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.
Watu
wasiopungua sita wameuawa katika hujuma hiyo huku wengine wawili
wakijeruhiwa baada ya gaidi aliyekuwa amejishehenesha mabomu kujiripua
katika mlango mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (NDS) mjini Kabul.
Hujuma
hiyo imetokea wakati wafanyakazi walipokuwa wakiwasili katika ofisi kwa
ajili ya kuanza kazi. Taarifa zinasema mwanamke mmoja ni miongoni mwa
waliouawa katika hujuma hiyo.
Wiki
iliyopita kituo kimoja cha Idara ya Usalama wa Taifa cha Afghanistan
kilishambuliwa na magaidi na katika makabiliano hayo magaidi watatu
waliuawa baada ya masaa matatu ya mapigano.
Hayo yanajiri wakati Mjumbe maalumu wa
rais wa Russia nchini Afghanistan akiwa ametoa indhari kuwa wanachama
zaidi ya elfu kumi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la ISIS hivi sasa
wako nchini Afghanistan na kwamba idadi yao inazidi kuongezeka kutokana
na kubadilisha maskani yake kundi hilo baada ya kusambaratishwa katika
nchi za Syria na Iraq.
Zamir
Kabulov ametoa indhari hiyo katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la
habari la Sputnik na kuongeza kuwa Russia ina wasiwasi wa kupanuka
harakati za ISIS kwenye mikoa ya kaskazini mwa Afghanistan inayopakana
na Tajikistan na Turkmenistan.
Ikumbukwe
kuwa hivi sasa kuna wanajeshi wapatao 11,000 wa Marekani nchini
Afghanistan. Washington na washirika wake katika muungano wa kijeshi wa
NATO waliivamia kijeshi nchi hiyo mwaka 2001 kwa kisingizio cha
kupambana na ugaidi lakini si tu kuwa hawajafanikiwa bali pia ugaidi
umeongezeka nchini humo.
China imezindua ndege ya "Jiaolong" AG600 ambayo ni ndege kubwa zaidi duniani inayoweza kutua nchi kavu na majini.
Ndege hiyo imeundwa kikamilifu
nchini China na jana ilifanikiwa kuruka kwa majaribio. Ndege hiyo ni kwa
ajili ya kukabiliana na ajali za moto misituni, na uokoaji watu majini.
Inaweza kuvuta maji tani 20 ndani ya sekunde 20, na kuzima moto katika
eneo la mita za mraba zaidi ya 4,000 mara moja, huku ikiweza kuwaokoa
watu 50 baharini mara moja. Mbali na kuzima moto na kuwaokoa watu, pia
inaweza kutumiwa katika uchunguzi na uhifadhi wa mazingira baharini.
Ndege hiyo pia inaweza kutumika kijeshi
na inatathminiwa kuwa uzinduzi wake ni katika jitiahda za China za
kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi.
Mapema mwaka huu, China ilizindua meli yake ya kwanza ya kivita yenye kusheheni ndege (aircraft carrier) iliyoundwa nchini humo.
Saudi Arabia ilimdhalilisha vibaya sana
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri katika safari yake ya hivi karibuni
mjini Riyadh wakati alipolazimishwa kusoma taarifa ya kujiuzulu mbele ya
televisheni.
Gazeti
la The New York Times limeandika Hariri alikuwa ni kama mateka na
alilazimishwa kusoma barua ya kujiuzulu akiwa sehemu isiyojulikana
Saudia mnamo Novemba 4 ambapo pia alitoa tuhuma zisizo na msingi kuwa
eti Iran na Hizbullah zinaingilia masuala ya ndani ya eneo na hivyo
amelazimika kujiuzulu.
Lakini
Rais wa Lebanon Michel Aoun alishuku kuwa Hariri alijiuzulu chini ya
mashinikizo na hivyo hakukubali hatua hiyo na alimtaka arejee nyumbani
kutoka Saudia. Vyombo vya usalama vya Lebanon vilithibitisha kuwa Hariri
alilazimishwa kujiuzulu na hatimaye alirejea Lebanon Novemba 22 baada
ya upatanishi wa Ufaransa. Hariri hatimaye alibatilisha uamuzi wake wa
kujiuzulu Disemba 5.
Taarifa zinasema kuwa Hariri
alipowasili Saudia alidhani atapokewa rasmi lakini alipofika katika
kasri ya mfalme alipokonywa simu zake za mkononi na walinzi wake
walitimuliwa huku wakitukanwa na maafisa wa usalama wa Saudia. Hapo
alikabidhiwa barua ya kujiuzulu na akaambiwa aisome katika televisheni
ya taifa ya Saudia. Badala ya kuenda hotelini alipelekwa katika nyumba
maalumu iliyokuwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa Saudia na wala
hakuruhusiwa kuonana na mke na watoto wake. Lengo la Saudia lilikuwa ni
kupunguza ushawishi wa harakati ya Hizbullah katika serikali ya Lebanon
lakini njama hizo zimegonga mwamba.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye moja ya harakati za kuripoti matukio kwenye eneo la Israel na Palestina
Waandishi wa habari 65 na wafanyakazi wa vyombo vya
habari wameuawa katika mwaka 2017, hii ni kwa mujibu wa ripoti
iliyochapishwa na shirika la wanahabari wasio na mipaka RSF.
Miongoni mwao 50 walikuwa ni maripota, hii ikiwa ni idadi ndogo zaidi katika kipindi cha miaka 14.
Hata hivyo ripoti
inasema kuwa huenda kupungua kwa idadi ya vifo vya wanahabari imetokana
na waandishi na ripota wengi kuacha kuripoti habari kwenye maeneo yenye
vita.
Nchi ya Syria ambao kwa
zaidi ya miaka 6 imeshuhudia vita vya wenywe kwa wenyewe, imesalia kuwa
nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari kufanya kazi, imeonesha ripiti
ya RSF ambayo imesema waandishi wa habari 12 waliuawa nchini humo,
ikifuatiwa na Mexico ambako 11 waliuawa.
Miongoni mwa waliouawa
nchini Mexico ni mwanahabari maarufu wa habari za biashara haramu ya
dawa za kulevya nchini humo Javier Valdez ambaye mauaji yake
yalitamausha wengi.
Waandamanaji nchini Kenya wakiwarushia mawe polisi na waandishi wa
habari, waliokuwa wakiripoti maandamano ya kupinga vitendo vya rushwa,
Nairobi, 3 Novemba, 2016.REUTERS/Thomas Mukoya
Mwandishi mwingine wa habari wa shirika la AFP aliuawa kwa kupigwa risasi nchini Mexico katika mji wa Kaskazini wa Sinaloa.
Nchi ya Ufilipino
imekuwa ni taifa jingine hatari kwenye ukanda wa Asia kwa waandishi wa
habari kufanya kazi ambapo ripiti inaonesha waandishi wa habari watano
waliuawa kwa kupigwa risasi mwaka uliopita.
Ongezeko hili lilitokana
na matamshi ya rais Rodrigo Duterte ambaye alisema “haimaanishi ukiwa
muandishi wa habari basi ndio usiuawe ikiwa unajihusisha na biashara
haramu”.
Hata hivyo hakukuwa na mwanahabari aliyeuawa mwaka uliotangulia nchini Ufilipino.
Waandishi wa habari nchini Misri wakiwa wamebeba kamera zao nje ya ofisi ya chama cha waandishi wa habari Reuters
Kiujumla ripoti ya RSF inasema kuwa idadi ya vifo vya wanataaluma wa habari imepungua kidunia katika kipindi cha miaka 14.
Katika vifo vya
wanahabari 65, ripoti inaonesha kuwa wanahabari 39 waliuawa huku wengine
wakipoteza maisha wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi kama vile
mashambulizi ya anga au yale ya kujitoa muhanga.
RSF inasema kuwa huenda pia vifo vimepungua kutokana na waandishi wengi wa habari kutopokea mafunzo ya kujilinda wakati wa vita.
Nchi ya Uturuki inatajwa
kwenye ripoti hii kwa kuwa na magereza mengi ambayo waandishi wa habari
wanashikiliwa, ambapo kwa sasa zaidi ya wanahabari 42 wanazuiliwa.
Nchi nyingine
zinazofunga waandishi wa habari kwenye jela zake ni pamoja na Syria
ambako kuna wanahabari 24, Iran wapo 23 na Vietnam ambako wako 19.
Rais JOSEPH KABILA pamoja na viongozi wa ngazi za juu
nchini DRC, waliokutana jijini GOMA tangu jumatatu wamehitimisha
mkutano wao usiku wa kuamkia leo huku wakiwataka raia wa nchi hiyo
kutojihusisha wala kujiunga na makundi ya waasi yanayotatiza usalama
kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
"Tumewaalika raia wa Congo kuilinda nchi yao piya twa
shukuru wana jeshi ambao hivi sasa wajitahidi katika ulinzi wa raïa
wilayani KASAI."
Huko magaavana walio shiriki mkutano huo walijulisha
umuhimu wa mazungumzo yao dhidi ya raïa wa Congo DRC, kama alivyo
julisha LOLA KISANGA liwali wa Jimbo la UELE.
"Twatazama yote tukiona jinsi gani usalama wa kweli waweza rejea na kusaidia kwa ujenzi bora wa nchi yetu"
Raia wamepokeaje yaliyo zungumziwa jijini Goma na viongozi serikali ya Congo DRC !
"Ikiwa hakuna upendo haya yote ni kupoteza mda.cha maana magavana hao watimize waliyo zungumza."
Licha ya kutozungumza na wanahabari kwenye mkutano
huo, duru za ndani zinaeleza kuwa rais Joseph Kabila aliwakosoa viongozi
ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wakati
huu wakijua anaelekea kumaliza muda wake.
Viongozi hao wa serikali ya Congo DRC wamethibitisha
kuendesha mkutano kama na huo jijini MBANDAKA mwezi machi mwaka ujao kwa
lengo la kuboresha zaidi uchumi na maendeleo ya jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo.
Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
zimekubaliana kuimarisha utaratibu wa mawasiliano na kupeana taarifa za
kiintelijensia kwa ajili ya kupambana na waasi wa ADF kufuatia
mashambulizi yao dhidi ya vikosi vya walinzi wa amani wa Umoja wa
Mataifa.
Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia
Richard Karemire amesema serikali ya Uganda na maofisa wa Kivu ya
Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa na mkutano wa
usalama.
Msemaji
huyo amesema kupeana taarifa kutasaidia vikosi vijiandae kuwazuia waasi
kujipenyeza ndani na mashambulizi yanayoweza kufanywa na ADF.
Hivi karibuni askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliuawa , 44 walijeruhiwa na wengine wawili hawajulikani walipo kufuatia hujuma ya waasi wa ADF.
Tukio hilo lilitokea Desemba 7,2017
katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini
mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu.
Askari waliouawa walikuwa ni sehemu
ya askari 3,000 wa tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa MONUSCO
yenye askari kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameashiria kufanyika Kikao cha Baraza la
Usalama la umoja huo kuhusu azimio nambari 2231 la mapatano ya nyuklia
ya Iran na kusema washiriki wa kikao hicho walitangaza kuunga mkono
mapatano hayo na kwamba kikao hicho kilithibitisha namna Marekani
ilivyotengwa.
Siku ya Jumanne, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
liliitisha kikao kujadili mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana
kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA yaliyofikiwa mwaka
2015 baina ya Iran na Russia, China, Uingereza, Ufaransa, Marekani na
Ujerumani. Baada ya mapatano hayo, Baraza la Usalama lilipasisha azimio
nambari 2231 kuhusu kuunga mkono utekelezwaji mapatano hayo.
Katika kikao cha Jumanne, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
Nikki Haley alitengwa na washiriki wote wa kikao wakiwemo Jeffrey
Feltman Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Joanne Adamson
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya ambao wote waliunga mkono JCPOA.
Akizungumza katika kikao hicho, Gholamali Khoshroo mwakilishi wa
kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisisitiza kuwa, Iran, kinyume
na Marekani, inafungamana kikamilifu na JCPOA na hilo limethibitishwa
katika ripoti 9 za Wakala wa Nyuklia wa Umoja wa Mataifa IAEA.
Mwakilishi wa Iran pia akijibu madai ya Nikki Haley katika kikao
hicho kuwa eti Iran inatoa msaada wa kijeshi kwa Yemen alisema:
"Mwakilishi wa Marekani anatoa tuhuma bandia dhidi ya Iran pasina
kuashiria namna harakati za kijeshi za serikali yake zinavyovuruga
uthabiti wa eneo kwa kuuza silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola na
kukabidhi baadhi ya silaha hizo kwa makundi ya kigaidi kama vile ISIS au
Daesh."
Katika kikao hicho Feltman pia amepinga madai hayo ya Haley.
Ikumbukwe kuwa tokea Machi 2015 hadi sasa, Marekani imekuwa ikiunga
mkono hujuma ya kinyama ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen na imekuwa ikiupa
utawala huo wa Riyadh silaha ambazo hadi sasa zimewaua Wayemen zaidi ya
13,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye
Umoja wa Mataifa amesema amestaajabishwa sana na kitendo cha jeshi la
Israel kumuua kwa kumpiga risasi mtu mwenye ulemavu aliyekuwa anaelekea
msikitini siku ya Ijumaa.
Zeid Ra'ad Al Hussein Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye
Umoja wa Mataifa ametoa kauli hiyo kufuatia ripoti kwamba mtu huyo
Ibrahim Abu Thurayeh aliuawa shahidi akiwa kwenye kitimwendo chake.
Ibrahim alikuwa miongoni mwa mamia ya Wapalestina walioandamana
Ijumaa karibu na uzio kati ya Ukanda wa Gaza na Israel, wakipinga hatua
ya Marekani kutambua mji wa Quds (Jerusalem) kuwa eti ni mji mkuu wa
utawala bandia wa Israel.
Zeid amesema taarifa zinadhihirisha kuwa jeshi la Israel lilitumia
nguvu nyingi kupita kiasi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za
kimataifa za kibinadamu.
Hili ni janga la pili kumkuta Ibrahim ambapo mwaka 2008 makombora yaliyorushwa na Israel yalimkataa miguu yake miwili.
Afisa huyo wa Umoja wa Maaifa ametaka hatua za kisheria zichuliwe dhidi ya waliotekeza jinai hiyo.
Mjumbe wa ngazi ya juu wa harakati ya
kupambana na biashara ya silaha nchini Uingereza amesema London inaiunga
mkono na kuihami Saudi Arabia na tawala nyingine kandamizaji duniani.
Andrew Smith ameliambia Shirika la Habari la Iran (IRNA)
kwamba, asilimia 60 ya silaha za Uingereza zinauzwa kwa tawala
zinazokiuka haki za binadamu na kwa watawala madikteta wa Mashariki ya
Kati.
Smith ameongeza kuwa, serikali kama ya Uingereza ambazo zimekuwa
zikimimina silaha katika maeneo yenye vita zinaiangalia maudhui hiyo kwa
mtazamo wa kibiashara ili ziweze kujikurubisha zaidi kwa tawala kama
Saudi Arabia na Bahrain.
Ameongeza kuwa Uingereza inaendelea kuiuzia silaha Saudi Arabia licha
ya mauaji na mgogoro mkubwa wa kibinadamu unaoshuhudiwa sasa nchini
Yemen ambao umesababishwa na mashambulizi na mzingiro wa serikali ya
Riyadh dhidi ya nchi hiyo.
Andrew Smith ameongeza kuwa, tangu mwanzoni mwa mgogoro wa Yemen,
Uingereza imeuizia Saudi Arabia silaha zenye thamani ya pauni bilioni 4
na milioni mia 600.
Vilevile harakati inayopinga biashara ya silaha nchini Uingereza
imewasilisha mashtaka dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Theresa May na kutoa wito wa kusitishwa mara moja mauzo ya silaha kwa
Saudi Arabia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza
kwamba Jamhuri ya Kiislamu itayawasilisha Umoja wa Mataifa madai ya
Nikki Haley, balozi wa Marekani katika umoja huo kwamba eti Iran
imeipatia silaha harakati ya Ansarullah ya Yemen.
Katika ujumbe wa baruapepe aliotuma kwa shirika la habari la
Russia la Sputnik, Dakta Zarif ameandika: Jamhuri ya Kiislamu
itawasilisha malalamiko Umoja wa Mataifa dhidi ya madai yaliyotolewa na
Marekani.
Siku ya Alkhamisi iliyopita, huku akiwa amesimama kando ya mabaki
kadhaa ya vyuma, Haley alianzisha propaganda mpya dhidi ya Iran kwa
kudai kwamba vyuma hivyo ni mabaki ya makombora ya Iran.
Pasi na kuashiria misaada ya silaha inayotolewa na Marekani kwa Saudi
Arabia, silaha ambazo zinatumika kuwashambulia raia madhulumu wa Yemen,
Haley aliituhumu Iran kuwa eti inaizatiti kwa silaha harakati ya
Ansarullah ya Yemen kwa ajili ya kuishambulia kwa makombora Saudia.
Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq ameyakanusha madai hayo yaliyotolewa na balozi wa Marekani katika umoja huo.
Kwa msaada na uungaji mkono wa Marekani, tangu mwezi Machi mwaka 2015
Saudi Arabia imeanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen na kuiwekea
nchi hiyo mzingiro wa ardhini, baharini na angani. Moto wa vita
uliowashwa na Saudia na waitifaki wake hadi sasa umesababisha makumi ya
maelfu ya watu kuuawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wengine kubaki bila
makaazi.
Muungano huo vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud
umekuwa kila mara ukidai kwamba Iran inavipatia vikosi vya wananchi wa
Yemen silaha na makombora na kwamba eti kwa kufanya hivyo inakwamisha
utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo.
Hata hivyo viongozi wa Yemen wamesisitiza mara kadhaa kuwa uwezo wa
kiulinzi na wa kujihami wa jeshi la nchi hiyo unatokana na nguvu zake za
ndani na kwamba licha ya mzingiro wa kila upande uliowekwa na utawala
wa Aal Saud, uwezo huo unaongezeka siku baada ya siku.
Utawala wa Aal Saud na Marekani hadi sasa zimeshindwa kufikia malengo
yao nchini Yemen ya kuwaweka vibaraka wao madarakani kutokana na
muqawama wa wananchi wa nchi hiyo.../
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
watoto UNICEF limeonya kuwa, zaidi ya watoto laki nne walio chini ya
umri wa miaka mitano wanakumbwa na utapiamlo mkubwa katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa ya Mfuko wa Watoto wa
Umoja wa Mataifa UNICEF imetahadharisha kuwa, watoto hao wanaweza
kufariki dunia katika kipindi cha miezi michache kutoka sasa kama hatua
za haraka hazitachukuliwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia watoto UNICEF limetangaza katikka taarifa yake kwamba,
mgogoro uliopo kwenye jimbo la Kasai na kudorora kwa shughuli za kilimo
ni sababu kubwa ya tatizo hilo.
Aidha shirika hilo la kimataifa limesema
kuwa, licha ya usalama kuboreka katika baadhi ya maeneo na hata raia
kuanza kurejea katika makazi yao, lakini hali ya kibinadamu bado ni
mbaya kutokana na kukosekana huduma muhimu.
Ripoti ya UNICEF inaonyesha kuwa, baadhi yya maeneo katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo hayana kabisa huduma za afya kutokana na baadhi
ya vituo kuporwa vifaa vyake au kuharibiwa.
Maeneo ya mashariki na kaskazini
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekuwa uwanja wa
mapigano na mauaji kwa miaka 20 sasa. Kushindwa jeshi la serikali na
askari wa kofia buluu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kukabiliana vilivyo
na waasi ni moja ya sababu kuu za kukosekana utulivu na amani katika
maeneo hayo kwa miaka 20 sasa.
Hata askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshindwa kuzima uasi nchini Mali
Duru za kiusalama za Mali zimetangaza kuwa
watu sita wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi
lililofanywa na watu wenye silaha katika mji wa Timbuktu wa kaskazini
mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Duru hizo zimesema, baadhi ya watu waliouawa ni wanachama wa kundi linalojulikana kwa jina la Tawariq.
Watu hao wameuawa baada ya gari lao
kushambuliwa na watu wenye silaha ambapo mbali na kuuawa watu sita na
kujeruhiwa wengine watatu, watu wengine wawili waliokuwemo kwenye gari
hiyo hadi hivi sasa hawajulikani waliko.
Nchi ya Mali ilikumbwa na machafuko tangu mwaka 2012 wakati
yalipotokea mapinduzi ya kijeshi na hapo hapo ukazuka uasi kaskazini mwa
nchi hiyo uliopelekea kutekwa na waasi, eneo kubwa la nchi hiyo.
Askari wa Umoja wa Mataifa pamoja na
wale wa mkoloni Ufaransa walitumwa nchini Mali katikati ya mwaka 2013,
lakini pamoja na hayo wameshindwa kuzima uasi huo licha ya kukomboa
baadhi ya maeneo yaliyokuwa yametekwa.
Licha ya kutiwa saini makubaliano ya
amani baina ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha ya kaskaizni mwa
nchi hiyo mwaka 2015, lakini machafuko bado yanaendelea huku mauaji ya
mara kwa mara na mashambulizi ya kushitukiza yakiripotiwa katika maeneo
tofauti ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Wananchi wa Mauritania wameungana na Waislamu
na wapenda haki katika kona zote za dunia kuendeleza maandamano ya
kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa hatua yake ya kuitambua Quds
kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
Mtandao wa gazeti la al Quds al
Arabi umetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, maeneo mbalimbali ya
Mauritania yameendelea kushuhudia maandamano ya kupinga uamuzi wa Trump
kuhusiana na mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas huku maelfu ya watu
walioshiriki kwenye maandamano hayo wakitoa nara za "Mauti kwa
Marekani," "Quds ni Yetu," "Mtake Msitake, Quds ni Mji Mkuu wa
Palestina" na "Hatutoruhusu Kuporwa Quds."
Watu wa matabaka mbalimbali nchini
Mauritania wametoa matamko wakiitaka serikali ya nchi hiyo na nchi
nyingine za Kiarabu na Kiislamu kukata uhusiano wao na Marekani kama
njia ya kupinga uamuzi wa Donald Trump wa kuitambua rasmi Baytul
Muqaddas kuwa kuwa eti ni mji mkuu wa Israel.
Donald Trump alitumia hotuba yake ya
siku ya Jumatano kufanya uchokozi wa wazi kwa kuitangaza Quds ambayo ina
Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa
Kizayuni na hapo hapo akatoa amri ya kuanza mchakato wa kuhamishiwa
Baytul Muqaddas, ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv, mji mkuu wa
utawala wa Kizayuni.
Viongozi wa nchi mbalimbali duniani nao
wamelaani hatua hiyo wakiwemo wa Ulaya kama Uingereza na Papa Francis,
kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani. Hata Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea
Kaskazini ameubeza uamuzi huo wa rais wa Marekani wa kuitangaza Quds
kuwa mji mkuu wa Israel na kusema kuwa, hakuna nchi inayoitwa Israel
hata Baitul Muqaddas uwe mji mkuu wake.
Wanawake wanaomtuhumu Rais Donald Trump wa
Marekani kwamba aliwanyanyasa kingono wamelitaka Bunge la nchi hiyo
(Kongresi) kufanya uchunguzi kuhusu kashfa za kimaadili za kiongozi
huyo.
Wanawake hao wanaosema walinyanyaswa kijinsia na Trump
walitarajiwa kukutana leo kwa mara ya kwanza na kutoa wito wa kuanza
uchunguzi kuhusu kashfa za kingono za Donald Trump.
Wakati
huo huo balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley amesema
kuwa wanawake wanaomtuhumu Rais Donald Trump kuwa aliwanyanyasa
kijinsia wanapaswa kuzikilizwa.
Haley amesema wanawake hao wanapaswa kusikilizwa na kesi yao inapaswa kushughulikiwa.
Gavana
huyo wa zamani na mmoja kati ya wanawake wenye vyeo vya juu katika
utawala wa Trump, amesema wakati umefika wa kutafakari kwa kina kuhusu
jinsi wanawake wanavyotendewa nchini Marekani.
Matamshi hayo ya balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
yanakwenda kinyume kabisa na sisitizo la serikali ya nchi hiyo ambayo
imekuwa ikidai kuwa kashfa za kuwanyanyasa kijinsia wanawake
zinazomkabili Donald Trump hazina msingi.
Makumi
ya wanawake wamemtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kuwa
aliwanyanyasa kingono ikiwa ni pamoja na kuwapapasa papasa, kuwabusu kwa
kuwalazimisha na kutumia maneno machafu na ya utovu wa maadili.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo
amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na masuala mengi tofauti
ikiwemo ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza hapa mjini Tehran,
suala la Quds, Yemen na masuala mengine mbalimbali.
Akijibu swali la mwandishi wa
Radio Tehran kuhusiana na ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza
hapa Iran ambayo imekwenda sambamba na hatua ya rais wa Marekani la
kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa Israel, Bahram Qassemi amesema, ziara
ya Boris Johnson waziri wa mambo ya nje wa Uingereza hapa Tehran ilikuwa
imepangwa tangu zamani na haina uhusiano wowote na hatua hiyo ya Donald
Trump.
Vile vile amesema, dunia nzima imeungana
hivi sasa kumlaani Donald Trump kwa hatua yake hiyo na nchi nyingi za
dunia zikiwemo za Kiarabu zinaendelea kukabiliana na uchokozi huo wa
rais wa Marekani kwa njia mbalimbali.
Amma kuhusiana na msimamo wa Iran kuhusu
Yemen, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
amesema, msimamo wetu kuhusu Yemen haujabadilika na hautobadilika,
kwanza sera zetu ni kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine lakini
pia tutaendelea kufanya juhudi za kuwatangazia walimwengu dhulma
wanayofanyiwa wananchi wa Yemen.
Amma kuhusiana na hatua ya Bahrain
kutuma ujumbe wake kwenda kuonana na viongozi wa utawala wa Kizayuni
katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Qasemi amesema, ziara
hiyo haina maana, ni kosa na ni kitendo cha aibu ambacho kimeonesha
sura halisi ya baadhi ya nchi za Kiarabu zinazoiunga mkono Israel
inayozikaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina kikiwemo Kibla cha Kwanza
cha Waislamu.