Serikali ya Nigerfia imetangaza kwamba, ina wasiwasi kuhusu silaha zinazoingizwa kwa wingi nchini humo kupitia njia za magendo.
Msemaji wa Idara ya Forodha ya Nigeria, Joseph Attah amesema
kuwa matokeo ya awali ya uchunguzi uliofanyika katika uwanja huo
yanaonesha kuwa, wahusika wa magendo ya silaha nchini Nigeria ni makundi
ya mafia yaliyoko nchini Uturuki.
Attah ameongeza kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu silaha zaidi ya
elfu tatu zimegunduliwa na kukamatwa katika bandari ya Lagos kutoka
Uturuki.
Hadi sasa ubalozi wa Uturuki nchini Nigeria haujasema lolote kuhusu
tuhuma hizo za magendo ya silaha kutoka Uturuki kelekea Nigeria.
Maafisa wa Idara ya Forodha ya Nigeria wanatazamiwa kufanya
mazungumzo na wenzao wa serikali ya Uturuki akiwemo balozi wa nchi hiyo
mjini Abuja kuhusu maudhui ya magendo ya silaha zinazoingizwa nchini
humo kutoka Uturuki.
Nigeria imekuwa ikisumbuliwa na machafuko makubwa hususan katika maeneo ya kaskasini mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment