
Mwanasheria Mkuu wa Kenya amesema kuwa nchi
hiyo haitakabiliwa na mgogoro wa kikatiba au wa kisiasa hata kama
uchaguzi rais wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26, umesogezwa
tarehe hadi baada ya mwishoni mwa Oktoba.
Githu
Muigai ameongeza kuwa, serikali ya sasa itaendelea kuwepo madarakani
kihalali kwa nguvu kamili ya kikatiba hadi uchaguzi mpya utakapokamilika
na kiongozi mpya kuapishwa.
Mahakama
ya Juu ya Kenya mwezi huu ilitengua ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta
katika uchaguzi wa Agosti 8 ikiashiria kuwepo kasoro na kuiamuru Tume
Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuandaa uchaguzi mpya hadi kufikia mwishoni
mwa mwezi Oktoba. Uhuru Kenyatta atachuana kwa mara nyingine na hasimu
wake kutoka muungano wa Nasa, Raila Odinga.
Mwanasheria
Mkuu wa Kenya alikuwa akijibu matamshi ya wakili wa Odinga katika
shauri lililopelekea kutenguliwa ushindi wa Kenyatta, Bwana James Orengo
aliyesema kuwa muhula wa urais wa Kenyatta utafikia kikomo iwapo
uchaguzi huo wa marudio hautafanyika hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba na
hivyo kuitumbukiza nchi katika mgogoro wa kikatiba.

No comments:
Post a Comment