Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemuita Rais
Donald Trump kuwa ni "ni mtu asiyeweza kufikiri sawasawa" na kusema
atalipa gharama kutokana na kauli zake za vitisho anazotoa dhidi ya nchi
hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini Kim Jong
Un amesema hii leo kuwa Trump ni mtu asiyestahili kuwa na hadhi ya kuwa
na mamlaka aliyo nayo ya amiri jeshi mkuu wa nchi na kumuelezea Rais
huyo wa Marekani kuwa ni mtu "mjanja na jambazi anayechezea moto".
Matamshi
hayo ya kiongozi wa Korea Kaskazini yanafuatia hotuba ya Rais Donald
Trump aliyoitoa katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne
wiki hii. Kim Jong Un amesema matamshi ya Trump yamemshawishi kuamini
kuwa njia ambayo kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliyochagua kuifuata
ni sahihi na kuwa ndiyo anapaswa kuifuata hadi mwisho na kuongeza kuwa
alikuwa akifikiria kuchukua hatua kali. Waziri wa mambo ya nje wa Korea
Kaskazini ameripotiwa akitishia nchi hiyo kufanya jaribio la bomu la
Hydrogen katika bahari ya pasifiki.
Trump atangaza vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini
Haya
yanakuja mnamo wakati Rais Donald Trump akitangaza vikwazo vipya dhidi
ya Korea Kasakazini vinavyolega kuidhibiti uwezo wa nchi hiyo katika
kuendeleza mipango yake ya kuwa na uwezo wa kutengeneza silaha za
nyukilia pamoja na makombora. Rais Trump alitangaza vikwazo hivyo hapo
jana wakati alipokuana na viongozi wa nchi washirika Japan na Korea
Kusini ikiwa ni siku mbili baada ya kulihutubia baraza kuu la Umoja wa
Mataifa na kutishia kuwa ataisambaratisha Korea Kaskazini iwapo
itaendelea na vitendo vyake vya uchokozi.
Trump
alisaini hapo jana amri nyingine ya utekelezaji inayolenga kuyapiga
marufuku makampuni yaliyoko Marekani yanayoshirikiana kibiashara na
Korea Kaskazini.
Waziri anayehusika na masuala
ya fedha wa Marekani Steven Mnuchin amesikika akisema kuwa taasisi za
fedha tayari zimetaadharishwa kuwa zinapaswa kuchagua moja ama zinafanya
biashara na Marekani au Korea Kaskazini.
Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchn
Tayari
Korea Kaskazini imeyapiga marufuku makampuni ya kigeni yanayoshirikiana
na Korea Kaskazini katika mipango yake ya kijeshi lakini hatua ya sasa
inatanua wigo wa vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini
ambavyo sasa vinagusa kuanzia teknolojia ya habari na mawasiliano, sekta
ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na viwanda vya nguo pamoja na uvuvi.
Hata
hivyo nyakati zitaeleza iwapo vikwazo hivyo vya kuchumi vitamlazimisha
kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kurudi nyuma ingawa kiongozi
huyo kijana anaonekana kuionyesha dunia kuwa hatishwi na matamshi makali
ya Trump.
Sigmar Gabriel asisitiza juu ya ushirikiano kimataifa
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel
Wakati
huohuo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel katika hotuba
yake kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa ameonya juu ya kauli za
kutanguliza masilahi ya taifa akionesha dhahiri kutokukubaliana na kauli
kama hiyo ambayo imetolewa mara kwa mara na Rais wa Marekani Donald
Trump.
Akizungumza pasipo kumtaja Trump,
Gabriel alisema kauli za kutanguliza utaifa kwanza ni kauli ambazo
zitasababisha migongano kitaifa na mwishowe hakuna faida
itakayopatikana. Amesisitiza kuwa dunia inahitaji ushirikiano zaidi
kimataifa na utaifa kidogo na siyo kinyume chake.
Aidha
waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alitoa mwito wa kuimarishwa
kwa Umoja wa Mataifa akitolea mfano wa mafanikio ambayo Ujerumani
imepata kupitia ushirikiano kimataifa na pia ushirikiano barani ulaya na
kuongeza kuwa halikuwa suala la "Ujerumani kwanza" lililoifanya
Ujerumani kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi bali ni Ulaya pamoja na
kuwajibika kimataifa.
No comments:
Post a Comment