Saturday, September 16, 2017

CHAMA TAWALA BURUNDI KIMELALAMIKIA RIPOTI YA UN KUHUSU HAKI ZA BINADU

Chama tawala nchini Burundi kimelalamiria ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyoitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ifanye uchunguzi kuhusu jinai zilizofanywa na viongozi wa Burundi dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Chama tawala Burundi jana kilieleza kuwa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayosema kuwa viongozi wa Burundi wamehusika katika kukiuka haki za raia wake kuwa ni ripoti ya kisiasa na yenye lengo la kutoa pigo kwa chama hicho tawala. 
Kuhusiana na suala hilo Evariste Ndayishimiye Katibu Mkuu wa chama tawala cha Burundi amezishambulia kwa maneno Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya  kufuatia ripoti hiyo yenye kukinzana dhidi ya viongozi wa Burundi na kuitaja Ulaya na nchi za magharibi kuwa ni mashetani wa Ulaya.
Evariste Ndayishimiye Katibu Mkuu wa chama tawala Burundi, CNDD-FDD  
Maafisa wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa tarehe Nne mwezi huu wa Septemba waliitaka mahakama ya ICC ichunguze jinai zilizofanywa na viongozi wa serikali ya Burundi dhidi ya raia wa nchi hiyo yakiwemo mauaji ya kunyonga nje ya mkondo wa sheria, utiaji mbaroni kiholela, mateso, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. Burundi ilitumbia katika mgogoro wa kisiasa tangu mwezi Aprili mwaka 2015 kufuatia hatua uya Rais Pierre Nkurtunziza wa nchi hiyo ya kuamua kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu kitendo ambacho kimepingwa na wapinzani wa Burundi wakisema kuwa ni kinyume na katiba. 

No comments:

Post a Comment