Monday, September 4, 2017

KIONGOZI WA CIA AMUONYA TRUMP KUTOKANA NA MATAMSHI YAKE MAKALI DHIDI YA KOREA KASKAZINI

Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA, Michael Hayden amemuonya Rais Donald Trump wa Marekani kutokana na kutoa matamshi makali dhidi ya Korea Kaskazini.
Michael Hayden ameyasema hayo leo Jumatatu na kuongeza kuwa, matamshi ya rais huyo wa Marekani dhidi ya Pyongyang, yanaweza kuzusha maafa makubwa. Kiongozi huyo zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA ameongeza kuwa, baadhi ya matamshi yaliyotolewa na Trump si ya mantiki. Kabla ya hapo Rais Donald Trump alitoa matamshi makali dhidi ya Korea Kaskazini akitishia kuishambulia kijeshi nchi hiyo ya Asia.
Michael Hayden, Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA
Matamshi na misimamo ya rais huyo wa Marekani imepelekea kuongezeka mgogoro katika eneo la Peninsula ya Korea. Kufuatia miamala hiyo ya Trump, serikali ya Pyongyang nayo imeendelea kujiimarisha kijeshi kukabiliana na chokochoko za Washington na washirika wake katika eneo hilo. Wakati huo huo, serikali ya China imeionya Korea Kaskazini juu ya hatua yake ya kuendelea kuyafanyia majaribio makombora yake ya balestiki. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China,  Geng Shuang amesema kuwa, Pyongyang haitakiwi kuifanya hali ya mambo katika eneo la Korea kuzidi kuwa mbaya zaidi na kwamba viongozi wa Korea Kaskazini ni lazima wafahamu kuwa, maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yamekataza mwenendo huo.
Geng Shuang , Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China
Kadhalika Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uchina amesisitiza kuwa, Beijing inatumai kwamba pande zote za mgogoro zitajizuia kutokana na hatua zinazoweza kuchochea zaidi mvutano katika eneo la Peninsula ya Korea.KIO

No comments:

Post a Comment