Monday, September 4, 2017

JESHI LA IRAN: TUTAEDELEZA KUZISAIDIA NCHI JIRANI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jenerali Muhammad Hossein Baqeri amesema kuwa Iran itaendelea kuzisaidia nchi majirani katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi.
Jenerali Hossein Baqeri ameyasema hayo leo katika maonyesho ya 'Mafunzo ya Umahiri" ya askari yaliyofanyika hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, licha ya kuwepo njama mbalimbali za adui na ukwamishaji mambo wa mabeberu wa dunia, lakini Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na uungaji mkono wa wananchi, imeendelea kupata mafanikio makubwa katika operesheni zake za kulinda usalama.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jenerali Muhammad Hossein Baqeri 
Aidha amesema kuwa, Iran ya Kiislamu imeendelea kutoa msaada kwa nchi majirani katika kukabiliana na ugaidi. Jenerali Hossein Baqeri amezungumzia maonyesho hayo na kusema kuwa mafunzo hayo ya umahiriyna lengo la kuwaweka tayari askari wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya vita yoyote wakati adui atakapoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Iran. Maonyesho hayo yamehudhuriwa na makamanda wa ngazi ya juu na viongozi mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapa mjini Tehran.

No comments:

Post a Comment