Wataalamu wa shirika la kutetea haki za
binadamu la Amnesty International wamesema kuwa, bomu lililoua raia 16
wa Yemen wakiwemo watu wote wa familia ya mtoto Buthaina aliyenusurika
shambulizi hilo, lilitengenezwa nchini Marekani.
Uchunguzi
uliofanywa na wataalamu wa silaha wa Amnesty International umebaini
kuwa, bomu lililotumiwa na Saudia kuua raia hao lina sifa za mabomu ya
Marekani yanayorushwa na ndege na kuongozwa kwa leza.
Ripoti
hiyo imesisitiza kuwa, mashambulizi yanayofanywa na Saudi Arabia na
washirika wake dhidi ya Yemen yanaendelea kuwa sababu kuu ya mauaji ya
raia hususan watoto wadogo nchini Yemen.
Matokeo hayo ya utafiti wa Amnesty International yametolewa baada ya
Umoja wa Ulaya kuwasilisha muswada katika Baraza la Haki za Binadamu la
Umoja wa Mataifa ukitaka kufanyike uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za
binadamu unaofanyika nchini Yemen.
Shambulizi
la ndege za Saudi Arabia lililofanyika tarehe 25 mwezi uliopita wa
Agosti katika makazi ya raia mjini Sana'a liliua raia 16 wakiwemo wazazi
wawili na mtoto Buthaina na ndugu zake watano. Alipoulizwa anataka
kufanya nini, Buthaina mwenye umri wa miaka 5 ambaye amebakia peke yake
kati ya watu wote wa familia yake, alisema anataka kurudi nyumbani na
kucheza na ndugu zake….
Picha zilizooneshwa na vyombo vya habari za mtoto huyo ndogo wa Yemen
aliyebakia peke yake baada ya familia yake yote kuuawa na ndege za
Saudi Arabia zimewasikitisha sana walimwengu.
Buthaina aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo amepoteza jicho lake moja.
No comments:
Post a Comment