Thursday, May 4, 2017

ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA WAPIGAKURA WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI WA RAIS IRAN

Uchunguzi wa maoni unaonesha kuwa, takriban asilimia 70.6 ya wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa 12 wa Rais humu nchini.
Asilimia takriban 63.5 ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB wameamua kuwa watashiriki katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu wa Mei na asilimia 7.1 wengine wamesema huenda wakashiriki kwenye uchaguzi huo.
Wagombea urais nchini Iran

Uchunguzi huo wa maoni umefanyika kwa kuwauliza maswali watu 38,000 walio na umri wa zaidi ya miaka 18 katika mji mkuu Tehran na katika miji mikuu ya mikoa ya Iran na pia katika miji mingine miwili yenye watu wengi pamoja na vijiji 10 kutoka katika kila mkoa wa Iran. Uchunguzi huo ulianza siku ya Jumapili na kumalizika juzi Jumanne (kuanzia Aprili 30 hadi Mei 2).
Asilimia takriban 23.6 ya waliojibu maswali waliyoulizwa wameamua hawatoshiriki na asilimia 1.2 wengine wamesema huenda wasishiriki. Asilmia 4.6 wengine wamesema hawajaamua iwapo watashiriki katika kupiga kura au la.
Grafu nayoonesha matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na IRIB kuhusu uchaguzi wa 12 wa rais wa Iran

Uchunguzi huo wa maoni umefanyika baada ya mjadala uliorushwa hewani mubashara kati ya wagombea sita wa urais, Ijumaa iliyopita na unaonesha kuongezeka idadi ya watu walioamua kushiriki kwenye uchaguzi baada ya mjadala huo.
Uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa na shirika la IRIB kabla ya mjadala huo ulikuwa umeonesha kuwa, asilmia 56.1 tu ya wapiga kura ndio waliokuwa na nia ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment