Tuesday, May 23, 2017

CHAMA TAWALA AFRIKA KUSINI CHAKANUSHA RIPOTI ZA KUJADILI KUMUONDOA MADARAKANI RAISI ZUMA

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimezitioa maanani na kueleza kuwa hazina ukweli ripoti za vyombo vya habari kwamba suala la kumwondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Jacb Zuma litajadiliwa katika mkutano muhimu wa chama hicho utakaofanyika mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa ANC Zizi Kodwa amekanusha ripoti hizo akisistiza kuwa ni za "kutunga na hazina ukweli".
Upinzani dhidi ya Zuma ndani ya chama tawala na kutoka vyama vya upinzani pamoja na makundi ya asasi za kijamii umeongezeka tangu kiongozi huyo alipomuuzulu waziri wa fedha anayeheshimika Pravin Gordhan mwezi Machi mwaka huu, hatua ambayo ilisababisha kushuka itibari ya kiuchumi ya Afrika Kusini.
Shirika la habari la Bloomberg limezinukuu duru mbili zikiripoti kuwa  ANC itajadili suala la kumwondoa madarakani Rais Zuma katika mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho utakaofanyika mwishoni mwa wiki, ripoti ambazo zimesababisha thamani ya sarafu ya nchi hiyo ya randi kupanda kwa asilimia 1.5 dhidi ya dola.
Pravin Gordhan
Rais Jacob Zuma, mwenye umri wa miaka 75, ambaye kipindi chake cha uongozi kinamalizika mwaka 2019, alinusurika na jaribio la ndani ya chama la kumwondoa madarakani mwaka 2016 baada ya Mahakama ya Katiba kutoa uamuzi kwamba alikiuka kiapo cha urais kwa kukataa kurejesha serikalini malipo ya fedha alizotumia kuboresha nyumba yake binafsi.
Zuma alihusishwa pia kwenye ripoti ya taasisi ya kupambana na ufisadi na tuhuma za kuruhusu jamaa wa familia moja ya wafanyabiashara wazaliwa wa India kuwa na ushawishi katika uteuzi wake wa baraza la mawaziri na katika zabuni zinazotolewa na makampuni ya serikali.
Hata hivyo kiongozi huyo na familia hiyo ya Gupta wamekanusha kutenda kosa lolote lile.../

No comments:

Post a Comment